Entertainment

Agnes Masogange akutwa na chembechembe za heroine na oxazepam

Agnes Masogange akutwa na chembechembe za heroine na oxazepam
Profile photo of sadock

Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali amesema mkojo wa mrembo Agness Gerald ‘Masogange’ umekutwa na chembechembe za dawa za kulevya aina ya heroine na oxazepam (Diacety Imophine).

Mkemia Elias Mulima (40) ameiambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kwamba sampuli ya mkojo wa Agness zilizowasilishwa kwao zilikua na chembechembe za dawa za kulevya.

Mulima ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi ya Masogange kukutwa na dawa za kulevya Februari 15, 2017 Dar es salaam akiongozwa na Wakili wa Serikali Constantine Kakula, Shahidi huyo amedai kuwa Februari 15 mwaka huu katika ofisi ya Mkemia mkuu Dar es salaam akiwa ofisini alipokea vielelezo kutoka Jeshi la Polisi vilivyowasilishwa na koplo Sospeter na WP Judith kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kubaini kuwa ni dawa za kulevya au la.

1468400693_7288_b

Pia shahidi huyo ameongeza kwa kudai kuwa iliwasilishwa na fomu maalumu ya dawa za kulevya ambayo ilikua na namba DCEA 008 na alifanya usajili na kuipa namba ya maabara 446/2017 ambapo Mshtakiwa alipewa kontena maalumu kwa ajili ya sampuli ya mkojo.

Pamoja na hayo Wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko alipinga kupokelewa kwa kielelezo hicho kwa sababu Polisi walitakiwa kuiomba Mahakama ili wachukue vipimo vya Mshitakiwa lakini hawakufanya hivyo na kudai ni kinyume na sheria 63 CPA.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28/2017 ambapo siku hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi wa kupokea ama kutopokea vielelezo vya sampuli ya mkojo wa Agnes Masogange kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

22637347_151631285443331_1675299238445056000_n

Picha: Rapper Gucci Mane afunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Keyshia Ka’oir

sadockOctober 18, 2017
luluuuu

Kesi ya mauaji bila kukusudia inayomkabili Elizabeth Lulu kuanza kusikilizwa wiki hii

sadockOctober 17, 2017
_98330961_4a22e640-0e79-444e-abc9-f7cb171064d0

Ed Sheeran apata ajali ya baiskeli, avunjika mkono

sadockOctober 17, 2017
maxresdefault (8)

Aslay: Huwezi nifananaisha na Diamond na Alikiba, nitajitahidi kuwafikia

sadockOctober 17, 2017