Entertainment

Alberto Msando ateuliwa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki na Waziri Mwakyembe

Alberto Msando ateuliwa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki na Waziri Mwakyembe
Profile photo of sadock

Baada ya kufanya vizuri kwenye kesi ya hakimiliki ya AY na Mwana FA dhidi ya kampuni ya Tigo, Alberto Msando amekula shavu serikalini.

Mwanasheria huyo na mdau wa masuala ya Sanaa, Alberto Msando ameteuliwa kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki na Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe.

Katika tarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara Bi Leah Kihimbi kuhusu uteuzi huo wa Msando imesema kwamba uteuzi huo umetokana na vikao vilivyofanywa na wadau wa sanaa pamoja Mh. Waziri Mwakyembe.

Msando-Uteuzi-1

Kwa upande wa Alberto Msando ambaye amepatiwa nafasi hiyo na serikali ameahidi kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria za nchi zinalinda haki za wasanii na kuhakikisha wasanii wanafaidika na kazi zao.

Msando ameandika  “Ulaya na Marekani wasanii wengi sio masikini. Hapa kwetu wasanii wengi ni majina tu. Wengi wanaishi maisha ya ‘naomba nitoe niko vibaya’. ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria zetu zinalinda haki za wasanii”.

Ameongeza “Harrison Mwakyembe tutafanya kazi uliyotutuma”

Msando mara nyingi amekuwa mbele katika kuwasaidia wasanii kwenye masuala yanayohitaji msaada wa kisheria.

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

chrissy-teigen-john-legend-selfie-getty

John Legend na mkewe Chrissy Teigen wanatarajia mtoto wapili

sadockNovember 22, 2017
huhuu

Tiwa savage: Mimi sio mjamzito, hizo ni taarifa za uongo

sadockNovember 22, 2017
clo1

Mkuu wa mkoa, Paul Makonda atembelea ofisi za Clouds Media Group kutoa pole

sadockNovember 22, 2017
pink-beautiful-trauma-tracklist

New Video: P!nk – Beautiful Trauma

sadockNovember 22, 2017