Entertainment

Baraka the Prince: Timu yangu ni Yanga tu, Alikiba namfahamu kama brother ambaye nipo naye lebel moja ya music

Baraka the Prince: Timu yangu ni Yanga tu, Alikiba namfahamu kama brother ambaye nipo naye lebel moja ya music
Profile photo of sadock

Kama ni mfatailiaji mzuri wa mitandao utakuwa umekutana na picha ya Baraka da Prince akiwa na Meneja wa Diamond, Babu Tale. Picha ambayo imezua maneno makubwa hasa kwasababu Baraka da Prince yupo lebel moja na Alikiba, Rockstar 4000.

Mashabiki wa Alikiba, TeamKiba wamemshutumu Hitmaker huyo wa Acha Niende kuwa msaliti kwa kujipendekeza kwa Diamond, pia wamedai Braka da Prince ana mpango wa kuamia kwenye lebel ya hasimu huyo mkubwa wa Alikiba, WCB.

princemtata

Kwa upande wa pili, Baraka da Prince amewashutumu mashabiki hao kwa kumpangia namna ya kuishi, huku akidai kuwa hana Timu yoyote, Timu pekee anayoshabikia ni Yanga,

“Mimi sinaga Timu mimi timu yangu ni Yanga, sinaga timu sijui nini sijui team nani sijui timu nani,” amesema. “Hizi timu za watu binafsi mimi sizifahamu sizijui kabisa. Mimi namfahamu Ali kama Ali kama brother angu ni mtu ambaye nipo naye kwenye record label moja tunafanya kazi tunafanya kazi.” Baraka alikiambia kipindi cha The Splash kinachoruka kupitia Ebony FM Radio.

Ameongeza, “Aaah Diamond pia namfahamu kama mtu wa karibu kwa hiyo mimi vitimu timu hivi.. unajua huwezi kumpangia mtu namna ya kuishi au aishi na nani afanye biashara na nani au akutane na nani kwa sababu mimi mwisho wa siku nina empire yangu mimi sijawahi kusema nataka sijui Team Barakah The Prince hata siku moja.”

idha msanii huyo anaendelea kutetea hoja zake ili Team Kiba wapate kuelewa ni nini anakihitaji katika maisha yake kwa sasa kupitia muziki.

“Kwa sababu mimi sitaki timu mimi nataka uwe shabiki yangu, uwe shabiki wa muziki wangu usiniingilie kwenye mambo yangu personal kwa sababu haujui pesa yangu naipata wapi na hujui nafanya nini naipata hela yangu ya muziki,” amesisitiza.

Barakah The Prince anaendelea kusisitiza, “We ni shabiki tu unataka niimbe kazi nzuri upende na u-enjoy tu ila hujui background yangu kuna nini kwahiyo sitaki chochote sijui kuhusu timu na ukijiona shabiki wangu wakutukana tafuta msanii mwingine wa kumshabikia.”

Kwa upande mwingine anatoa ushauri kwa mashabiki wote wa muziki wa Bongo Flava. “Kwahiyo kama ni shabiki yangu na mimi si msanii wa Bongo Flava kwanini usifanye kuwa shabiki pia wa Diamond, kwa nini usimsapoti pia Alikiba au kwanini usimsapoti Ben Pol wewe unataka kuleta timu ili iweje? Mimi sihitaji gemu yangu haiko hivyo nafanya good music na type pia ya mashabiki zangu ukiona shabiki yoyote anatukana matusi kwenye internet huyo sio shabiki yangu sitaki mashabiki wa kutukana sitaki mashabiki wap*mbavu.”.

Hata hivyo Barakah The Prince anafafanua zaidi aina ya mashaniki wake, “Nina mashabiki watu wazima, ndio maana kwenye ma-event mpaka Bungeni wapi naitwa sometimes kwa sababu naimba muziki ambao kila mtu anaweza kuusikiliza watoto, akina Mama, Wazee na Vijana.”

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017
Vanessa Mdee

Vanessa Mdee asaini mkataba mnono na Universal Music Group, kusimamia usambazaji wa kazi zake nje

sadockDecember 20, 2017