Hot Below Trending

Barcelona yashindwa kupata bao kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano

Barcelona yashindwa kupata bao kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano
Profile photo of sadock

Barcelona walilazimishwa sare 0-0 na klabu ya Olympiakos na hivyobasi kushindwa kufunga bao kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano katika mechi ya kimakundi ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Luis Suarez alipiga mwamba wa goli huku Barcelona ikijaribu kutafuta ushindi ambao ungewasaidia kufuzu katika raundi ya muondoano huku ikiwa imesalia mechi mbili.

Baadaye mshambuliaji huyo alimpgia pasi Lionel Messi badala ya kufunga yeye mwenyewe baada ya saa moja.

Barca inaongoza kundi D kwa pointi tatu baada ya Juventus kupata sare ya 1-1 na Sporting Lisbon.

Ernesto Valverde ambaye alikuwa anarudi kwa klabu yake ya zamani aliisaidia timu yake kupata alama 10 katika mechi nne.

Barca inahitaji pointi moja pekee kutoka kwa mechi mbili za mwisho dhidi ya Juventus na Sporting kufuzu katika raundi ya timu 16.

Juventus ambayo imeshinda mechi mbili, kupata sare moja na kupoteza mechi moja iko pointi tatu juu ya Sporting Lisbon ambayo ipo katika nafasi ya tatu.

Gonzalo Higuain alisawazisha ikiwa imesalia dakika 11 baada ya Bruno Cesar kuiweka kifua mbele Sporting Lisbon uongozini baada ya kipindi cha kwanza .

Juve sasa ipo katika nafasi nzuri kusonga mbele katika raundi ya timu 16

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017