Entertainment

Beyonce aongezwa kwenye cast ya toleo jipya la ‘The Lion King’

Beyonce aongezwa kwenye cast ya toleo jipya la ‘The Lion King’
Profile photo of sadock

Disney wametoa orodha ya mastaa watakao ingiza sauti zao katika toleo jipya la filamu ya animation ya ‘The Lion King’. Beyonce ni mmoja ya mastaa waliotangazwa kushiriki.

Mwezi Machi mwaka huu, Variety iliripoti kuwa mrembo huyo mwenye watoto watatu amekuwa chagua la kwanza kwa Disney ambao ni waandaaji wa filamu hiyo.

LIONKING

Kupitia mtandao wa Twitter, Disney wameweka picha za waigizaji ambao watashiriki katika filamu hiyo mmoja wapo ni Queen Bey ambaye ametumia jina la Nala.

Washiriki ambao watakuwepo katika The Lion King ni pamoja na Donald Glover (Simba), James Earl Jones (Mufasa), Chiwetel Ejiofor (Scar), Alfre Woodard (Sarabi), Seth Rogen (Pumbaa), Eric Andre (Azizi), John Oliver (Zazu), John Kani (Rafiki), and Billy Eichner (Timon).

Filamu hiyo inatarajiwa kutoka katika kipindi cha majira ya joto mwaka 2019.

 

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

chrissy-teigen-john-legend-selfie-getty

John Legend na mkewe Chrissy Teigen wanatarajia mtoto wapili

sadockNovember 22, 2017
huhuu

Tiwa savage: Mimi sio mjamzito, hizo ni taarifa za uongo

sadockNovember 22, 2017
clo1

Mkuu wa mkoa, Paul Makonda atembelea ofisi za Clouds Media Group kutoa pole

sadockNovember 22, 2017
pink-beautiful-trauma-tracklist

New Video: P!nk – Beautiful Trauma

sadockNovember 22, 2017