Entertainment

Chid Benz: Nimetoka Cuba kufanya collabo na 2Pac, nitamleta Bongo siku chache zijazo

Chid Benz: Nimetoka Cuba kufanya collabo na 2Pac, nitamleta Bongo siku chache zijazo
Profile photo of sadock

Rapper maarufu Bongo, Chid Benz ameibuka na kusema kuwa amefanya collabo na rapper mkongwe wa Marekani, marehemu Tupac Shakur huku akiapa kumleta Bongo.

Chid Benz ambaye pia alikanusha kukamatwa na kutumia Dawa za Kulevya alidai kuwa amekuwa akiongea na rapper huyo wa Marekani na tayari wamerekodi hadi vipande vya video kwa ajili ya comeback yake.

“Tupac yupo hai, yupo Cuba, nilienda Cuba juzi juzi alinipigia simu nionane nae, anataka kurudi kwenye game na kuonesha yupo hai kwahiyo alinipiga akaniuliza mwanangu Chid tunafanyaje, nikamwambia tusifanye ngoma kwanza tufanye ki’movie kwanza” Chid Benz alifunguka kwenye ENewz ya EATV.

Tupac atakuja Bongo, nitawaita mfanye nae interview, nitakuwa nae chanika kule. Kuna mpango nae wa ngoma tayari nimesha mtumia beat kwa Mensen Selekta pale, kafanya verse moja, na mimi moja nafakiria kutafuta mtu wa kufanya Chorus” Chid Benz alisisitiza.

Tupac Shakur alifariki dunia baada ya kupigwa risasi tarehe 13 septemba mwaka 1996 jijini Las Vegas alipokuwa akitoka kwenye pambano la Mike Tyson na Bruce Seldon.

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

mgid_ao_image_logotv

New Video: Jennifer Hudson – Burden Down [Official Music Video]

sadockDecember 13, 2017
_99171871_cef98067-831f-46ed-9b08-b20ac967d873

Oscar Pistorius apata majeraha baada kupigana gerezani

sadockDecember 13, 2017
eminem-e1507948158888-825x620

Eminem: Huwa narekodi ngoma zaidi ya 50 ili nipate ngoma 20 bora kwa ajili ya Album

sadockDecember 11, 2017
WAKADR

Waka ya Diamond yashiKa namba 1 Tanzania, Kenya na Uganda kwenye mtandao wa YouTube

sadockDecember 11, 2017