Hot Below Trending

Cristiano Ronaldo amfunika tena Messi kwenye tuzo ya Ballon D’or

Cristiano Ronaldo amfunika tena Messi kwenye tuzo ya Ballon D’or
Profile photo of sadock

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Mreno Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka wa pili mfululizo usiku wa kuamkia leo.

Ronaldo amemshinda mpinzani wake wa karibu Lionel Messi, katika tuzo hiyo na kuweza kuitwaa kwa mara ya tano na kuwa sawa na Messi ambae pia ametwaa kwa mara tano.

FIFA-Ballon-dOr-Gala-2014

Nyota wa Barcelona Lionel Messi, amepata nafasi ya pili huku mchezaji mahiri wa Psg ya nchi Ufaransa Neymar Jr,akiwa katika nafasi ya tatu

Msimu uliopita Ronaldo aliisaidia timu yake ya Real Madrid kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya na ubingwa wa la Liga kwa mara ya kwanza toka toka mwaka 2012.

Ballon d’Or ni tuzo ambayo imekua ikitolewa na jarida la nchini Ufaransa toka mwaka 1956 na kura hupigwa na waandishi wa habari wapatao 173, duniani kote.

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017