Entertainment

Diamond amtambulisha rasmi Marombosso wa Yamoto Band kujiunga WCB

Diamond amtambulisha rasmi Marombosso wa Yamoto Band kujiunga WCB
Profile photo of sadock

Staa wa muziki wa Bongo Fleva na mmiliki wa lebo ya muziki ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz amemaliza utata wa kilichokuwa kikisemekena chini kwa chini kuhusu mmoja kati ya wasanii waliounda Bendi ya Yamoto ‘Maromboso’ kudaka dili la kufanya kazi chini ya Usimamizi wa leo ya WCB Wasafi.

Kupitia ukurasa wa Instagram katika kumtakia heri ya tarehe ya mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Maromboso, Diamond amethibitisha kuwa ni muda muafaka tu unaosubiriwa kubayanisha kuwa muimbaji Maromboso atafanya kazi rasmi kama msanii chini ya usimamizi wa lebo kama inavyofanyika kwa wasanii wengine kama vile Rich Mavoko, Harmonize, Lava Lava, Ray Vanny na Queen Darleen.

mbosssos

Taarifa ambazo hazikuwa na uhakika kuhusu Maromboso kuanza kufanya kazi na lebo ya muziki ya WCB Wasafi zilianza kukolea zaidi kipindi ambacho Kundi la muziki la Yamoto Bendi lilipoanza kuingia katika sura ya kuvunjika kwa mfumo wa kila msanii aliyeunda Bendi hiyo kufanya kazi zake binafsi ambapo baadae Maromboso alitokea katika wimbo wa ‘Zilipendwa’ uliowashirikisha wasanii wote wa lebo ya WCB huku amshabiki wengi wao walijijazia majibu wenyewe kuwa Maromboso ameanza kufanya kazi na lebo hiyo.

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

mgid_ao_image_logotv

New Video: Jennifer Hudson – Burden Down [Official Music Video]

sadockDecember 13, 2017
_99171871_cef98067-831f-46ed-9b08-b20ac967d873

Oscar Pistorius apata majeraha baada kupigana gerezani

sadockDecember 13, 2017
eminem-e1507948158888-825x620

Eminem: Huwa narekodi ngoma zaidi ya 50 ili nipate ngoma 20 bora kwa ajili ya Album

sadockDecember 11, 2017
WAKADR

Waka ya Diamond yashiKa namba 1 Tanzania, Kenya na Uganda kwenye mtandao wa YouTube

sadockDecember 11, 2017