Entertainment

Diamond Platnumz: Sijawahi kulipia collabo yoyote na msanii wa Marekani

Diamond Platnumz: Sijawahi kulipia collabo yoyote na msanii wa Marekani
Profile photo of sadock

Staa wa Bongo Fleva, Diamond amefunguka kuwa hajawahi kumlipa msanii yoyote wa Marekani kufanya nae collabo, huwa inatokea wanaelewana tu.

“Mimi sijawahi kulipa kolabo yoyote kwanza ya Marekani niliyowahi kufanya, sijawahi kulipa na ukichunguza kiundani kolabo zangu na Wamarekani siyo kitu ambacho ‘nimejishobokesha’ ni watu wenyewe ambao wanatokea kunikubali na kuupenda muziki ambao ninaufanya,” Diamond alifunguka alipokuwa akihojiwa na Dizzim Online.

OMARION

“Ndio maana unaona sometimes sipost naona kama sina haja ya kupost ikiwa wao wenyewe wanakuwa wanafurahi na wanapenda kupost kitu tunachokifanya. Sometimes naogopa kupost naonekana kama nitajishauwa, sitaki kuonekana hivyo, nataka nionekane pointi yangu kuuchukua muziki wa Tanzania kuupeleka mbali.” Aliongeza.

Milango ya collabo za wasanii wa Marekani imemfungukia staa huyo wa Hallelujah ukiachana na ile ya Neyo ambayo tayari ilishatoka, Diamond anacollabo nyingine na Rick Ross na nyingine na Omarion ambazo zipo tayari na video ameshashoot.

 

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

chrissy-teigen-john-legend-selfie-getty

John Legend na mkewe Chrissy Teigen wanatarajia mtoto wapili

sadockNovember 22, 2017
huhuu

Tiwa savage: Mimi sio mjamzito, hizo ni taarifa za uongo

sadockNovember 22, 2017
clo1

Mkuu wa mkoa, Paul Makonda atembelea ofisi za Clouds Media Group kutoa pole

sadockNovember 22, 2017
pink-beautiful-trauma-tracklist

New Video: P!nk – Beautiful Trauma

sadockNovember 22, 2017