Hot Below Trending

Donald Trump atoa onyo kali kwa Korea Kaskazini ‘Usitujaribu’

Donald Trump atoa onyo kali kwa Korea Kaskazini ‘Usitujaribu’
Profile photo of sadock

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa onyo kali kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un katika hotuba ndani ya bunge la Korea Kusini.

”Usitudharau, Usitujaribu,” alisema, huku akishutumu hali ilivyo nchini Korea Kaskazini.

Bwana Trump alimzungumzia moja kwa moja rais Kim akisema kuwa ”silaha unazojilimbikia hazikufanyi wewe kuwa salama lakini zinakuweka katika hali hatari”.

Kiongozi huyo wa Marekani yuko katika ziara ya siku mbili nchini Korea Kusini katika ziara ya bara Asia.

Kwengineko katika hotuba yake amesema kuwa huku Korea Kaskazini ikiona uvumilivu kuwa udhaifu sasa kuna utawala mpya nchini Marekani.

Bwana Trump pia ameutaka ulimwengu hususan China na Urusi kuiwekea shinikizo kali Pyongyang kusitisha utengenezaji wake wa silaha za kinyuklia.

Dunia haiwezi kuvumilia hatari inayosababishwa na taifa linaloongozwa na utawala usioaminika ambao unaitishia na silaha za kinyuklia.

Mataifa yote yaliowajibika yanafaa kuungana kuangamiza utawala wa kikatili wa Korea Kaskazini kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeuunga mkono, kupata usaidizi wowote ama hata kukubalika, alisema.

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017