Hot Below Trending

Donald Trump awajia juu CNN “Mnaichafua Marekani nje ya nchi”

Donald Trump awajia juu CNN “Mnaichafua Marekani nje ya nchi”
Profile photo of sadock

Rais wa Marekani, Donald Trump amelishambulia Shirika la Habari la CNN kwa maneno akiwambia kuwa wameshindwa kuwa wazalendo kwa kuandika habari za uongo.

Rais Trump amesema CNN ni kituo kinachoaminiwa nje ya Marekani lakini cha kushangaza ndani ya Marekani kituo hicho kimekosa ushawishi huku akidai kuwa huenda kikaharibu sifa ya Marekani nje ya nchi.

Fox ni kituo muhimu sana kwa taifa la Marekani kuliko CNN. Lakini nje ya Marekani watu wanaiamini sana CNN, ingawaje habari zao zote sio za kweli, Mbaya zaidi wanaiwakilisha taifa letu kwa habari za uongo. Na wanaaminiwa sana na watu wa nje wahajui ukweli.“ameandika Rais Donald Trump kwenye ukurasa wake wa Twitter na kudai kuwa kama kungekuwa na tuzo za Media inayotoa habari feki basi CNN wangepewa.

Tunapaswa kuwa na ushindani kwenye makampuni yetu ya habari ikiwemo CNN ila sio Fox (akimaanisha FOX pekee ndio wanaoandika habari za uhakika), Hawa CNN sio waaminifu, wala rushwa na wanamchafua Rais (Donald Trump) kwenye habari zao. Vyombo vyote vya habari ni vibaya, natumaini mshindi atahitaji taji la Uandishi wa Habari za uongo.“ameandika Rais Donald Trump.

Hata hivyo CNN kupitia ukurasa wao wa Twitter wamemjibu Rais Trump kwa kumwambia kuwa hao jukumu lao ni kutoa habari na sio kuiwakilisha Marekani nje ya nchi kwani hilo ni jukumu la Rais.

Hii sio mara yake ya kwanza Rais Donald Trump kuwashambulia CNN kwani mapema mwezi Julai mwaka huu Trump aliposti picha akimshambulia muandishi wa Habari mwenye Mic ya CNN.

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017