Hot Below Trending

Idadi ya watu waliouawa kwenye shambulizi Mogadishu yafika 300

Idadi ya watu waliouawa kwenye shambulizi Mogadishu yafika 300
Profile photo of sadock

Idadi ya watu waliouawa kwenye ,lipuko mkubwa wa bomu katika eneo lenye shughuli nyingi kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumamosi, imefikia watu 300 hadi sasa, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la hahari la Reuters

Takriban watu wengine 300 walijeruhiwa kwa mujibu wa AFP, wakati lori lililokuwa limejazwa milipuko lilipolipuka karibu na lango la hoteli.

_98328507_15035f78-7bf2-4b43-9471-32f924619bff

Reuters walimnukuu Ahmed Ali, muuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja akisema kuwa miili 160 haikuweza kutambuliwa na hivyo ilizikwa na serikali jana. Anasema kuwa miili mingini iliziwa na jamaa zao.

Hilo ndilo shambulizi baya zaidi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007.

Rais Mohamed Abdullahi “Farmajo” Mohamed alilaumu kundi la al-Shabab kwa shambulizi hilo katili.

“Tumethibitisha kuwa watu 300 waliuawa kwenye mipuko huo. Idasi ya waliokufa huenda bado ikaongezeka na kuna watu kadha ambao bado hawajulikani waliko,” Abdikadir Abdirahman, mkurugenzi wa idara ya magari ya kusafirisha wagonjwa aliliambia shiria la Reuters.

 

BBC Swahili

 

 

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

chrissy-teigen-john-legend-selfie-getty

John Legend na mkewe Chrissy Teigen wanatarajia mtoto wapili

sadockNovember 22, 2017
huhuu

Tiwa savage: Mimi sio mjamzito, hizo ni taarifa za uongo

sadockNovember 22, 2017
clo1

Mkuu wa mkoa, Paul Makonda atembelea ofisi za Clouds Media Group kutoa pole

sadockNovember 22, 2017
pink-beautiful-trauma-tracklist

New Video: P!nk – Beautiful Trauma

sadockNovember 22, 2017