Hot Below Trending

Jose Mourinho: Sina mpango wa kuhamia PSG

Jose Mourinho: Sina mpango wa kuhamia PSG
Profile photo of sadock

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amekana uvumi unaoenea kwamba huenda akahamia PSG.

Raia huyo wa Ureno aliambia chombo cha habari siku ya Jumapili kwamba hatomaliza kazi yake ya ukufunzi katika uwanja wa Old Trafford na kwamba ni kocha mwenye maono na kwamba anapendelea kufanya mambo mapya.

Alipoulizwa kuhusu matamshi yake siku ya Jumanne alisema kwamba haondoki.

‘Sisaini mkataba mpya wa miaka mitano na pia siamiii PSG” alisema Mourinho mwenye umri wa miaka 54.

35F7CA0F00000578-3674838-image-a-34_1467715967418

Katika mahojiano ya Jumapili, Mourinho ambaye aliisifu klabu hiyo ya Ufaransa na kwamba mwanawe alipendelea kwenda kutazama mechi ya klabu hiyo badala ya ile ya Manchester United.

Kwa nini Paris? Kwa kuwa kuna kitu maalum. Mchezo mzuri, ubora, ujana ni vitu vya ajabu , alisema.

Akizungumza kabla ya mechi ya vilabu bingwa ugenini Benfica, Mourinho alijibu kwamba vyombo vya habari vya Uingereza vina jibu.

”Kwa sababu kwa siku moja ninaambiwa kwamba nitatia saini kandarasi ya miaka mitano ilio na thamani ya £1bn na siku nyengine munasema kuwa ninaondoka na kuelekea PSG”.

Nadhani hilo ndio jibu, jibu ni kwamba hakuna kinachofanyika. Mourinho ambaye yuko katika msimu wake wa pili na Red Devils hajawahi kufanya kazi kwa zaidi ya miaka minne katika klabu moja.

 

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017