Entertainment

Kesi ya mauaji inayomkabili Elizabeth Michael yaanza kusikilizwa mahakama kuu leo

Kesi ya mauaji inayomkabili Elizabeth Michael yaanza kusikilizwa mahakama kuu leo
Profile photo of sadock

KESI inayomkabili mwigizaji maarufu wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa staa wa filamu nchini, Steven Kanumba imeanza kuunguruma tena leo Alhamisi, Oktoba 19 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Jaji Sam Rumanyika, ushahidi upande wa Jamhuri ulitolewa na mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco,  ambaye alikuwa shahidi wa kwanza.

Akijibu swali la wakili wa utetezi, Peter Kibatala, shahidi Seth ameieleza mahakama hiyo juu ya ugomvi alioushuhudia kati ya Elizabeth Michael na marehemu Steven Kanumba siku ya tukio.

LULU

Seth  ameieleza mahakama kwamba anachofahamu yeye ni kuwa palikuwa na mgogoro kati ya Lulu na Kanumba aliousikia, uliosababishwa na simu kwamba, Lulu alikuwa akiongea kwa simu na mwanaume mwingine hali iliyozua ugomvi huo.

Mbali na Seth, shahidi wa pili aliku,,wa ni daktari ambaye hata hivyo hakufika mahakamani hapo kwa kuwa aliomba udhuru kwa madai kuwa anaumwa. Jaji Rumanyika ameiahirisha kesi hiyo hadi kesho saa tatu. Mashahidi waliobaki ambao ni watatu watatoa ushahidi wao.

Baadhi ya watu waliofika kusikiliza kesi hiyo ni mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila, mama mzazi waKanumba, Flora Mtegoa, muigizaji Dkt. Cheni na wengine.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo cha Kanumba bila kukusudia, mnamo Aprili 7, 2012 .

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017
Vanessa Mdee

Vanessa Mdee asaini mkataba mnono na Universal Music Group, kusimamia usambazaji wa kazi zake nje

sadockDecember 20, 2017