Pick of the day

Kim Jong-un akabidhiwa mpango wa kushambulia Guam

Kim Jong-un akabidhiwa mpango wa kushambulia Guam
Profile photo of sadock

Kiongozi wa Korea Kaskazini amepokezwa habari kuhusu mpango wa taifa hilo wa kutaka kurusha kombora hadi katika kisiwa cha eneo la pacific cha Guam kinachomilikiwa na Marekani kulingana na ripoti za vyombo vya habari.

Lakini ripoti hiyo imesema kuwa itachunguza vitendo vya Marekani kabla ya kuchukua hatua ya kurusha kombora hilo katika kisiwa cha Guam.

Wiki iliopita, Korea Kaskazini ilionya kwamba mikakati inawekwa kushambulia eneo ambalo ndege za kijeshi za Marekani zimekita kambi.

Kumekuwa na cheche za maneno kati ya Marekani na Korea kaskazini.

Ripoti hiyo ya kitengo cha habari cha KCNA ilisema kuwa Kim Jong un aliutazama mpango huo kwa muda mrefu na kuujadili na maafisa wakuu wa jeshi.

Kamanda wa jeshi la kimkakati la Korea Kaskazini sasa anasubiri agizo baada ya kuandaa shambulio hilo la Guam.

Lakini ripoti hiyo pia imeongezea kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini atachunguza mienendo ya Marekani kabla ya kutoa uamuzi wowote, hatua inayoonekana kupunguza kasi ya cheche za maeneo kati ya mataifa hayo mawili.

Mwandishi wa BBC Yogita Limaye mjini Seoul anasema kuwa hatua hiyo itapunguza wasiwasi na kuzuia mgogoro wa kijeshi katika eneo la Korea.

Mwandishi mwengine ameongeza kuwa baada ya siku kadhaa za vitisho kutoka Pyongyang ,inaonekana kwamba rais Kim Jong Un sasa anataka kunyamaza na kutazama hali ,lakini katika taifa lenye siri kubwa kama Korea Kaskazini huwezi kuwa na hakika.

Wachanganuzi wanasema inamaanisha kwamba Pyongyang haiko tayari kutekeleza shambulio katika kisiwa cha Guam, kwa hivyo huenda inachukua muda.

_97333192_guam_map624

Hatua hiyo inajiri baada ya waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis kuonya kwamba shambulio lolote linaweza kusababisha vita vikali, na iwapo Pyongyang itarusha kombora kuelekea Guam basi ”itakuwa vita”.

Ameambia maripota kwamba Jeshi la Marekani litatetea taifa hilo kutoka kwa shambulio lolote wakati wowote na kutoka kwa taifa lolote.

Pia aliwahakikisha raia wa Guam ,ambapo kuna kambi za kijeshi za Marekani kwamba takriban watu 160,000 wanalindwa na akasema iwapo kombora litarushwa ”tutalitibua”.

BBC Swahili

Comments

comments

Pick of the day

More in Pick of the day

Robert-Mugabe

Rais Robert Mugabe atangaza amejiuzulu

sadockNovember 22, 2017
beyonce-smile-brit-awards-billboard-1548

Beyonce aongoza orodha ya Forbes ya Mastaa wa kike kwenye muziki waliongiza mkwanja mrefu zaidi 2017

sadockNovember 21, 2017
robert_mugabe_0

Bunge la zimbabwe kuamua hatma ya Mugabe leo

sadockNovember 21, 2017
american-music-awards-logo-620x360

American Music Awards 2017: Orodha kamili ya washindi

sadockNovember 20, 2017