Entertainment

Lupita asimulia alivyofanyiwa unyanyasaji wa kingono na mtayarishaji mkubwa wa filamu duniani Harvey Weinstein

Lupita asimulia alivyofanyiwa unyanyasaji wa kingono na mtayarishaji mkubwa wa filamu duniani Harvey Weinstein
Profile photo of sadock

Muiguizaji mwenye asili ya Afrika Lupita Nyong’o amedai alitaka kufanyiwa unyanyasaji wa kingono na mtayarishaji mkubwa wa filamu duniani Harvey Weinstein.

Lupita amelieleza gazeti la  New York Times, kuwa amewahi kufanyiwa unyanyasaji huo na Weinstein ambaye walikutana mwaka 2011, katika sherehe za ugawaji tuzo mjini Berlin, Ujerumani kipindi bado ni mwanafunzi katika shule ya uigizaji ya Yale School of Drama.

Mrembo huyo ameeleza kuwa alitambulishwa na rafiki yake kwa Weinstein, na aliambiwa akae karibu  na mwanaume huyo ili aweze kufanikiwa katika taaluma yake uigizaji. Lupita ameeleza kuwa baada ya muda kupita alialikwa na mwanaume huyo nyumbani kwake kwa ajili ya kumuunganisha katika dili za kucheza filamu.

483042217-600x743

“Nilifika nyumbani kwa Weinstein, nikakutana na mke wake na watoto wake na kisha akaenda kuandaa chumba binafsi kwa ajili ya kutazama filamu. Baada ya dakika 15 Weinstein alirejea sebuleni na kunialika katika chumba hicho binafsi.” ameeleza Lupita.

Akaongeza “Baada ya kufika chumbani humo Harvey aliniomba nimfanyie massage, akajiandaa kwa ajili ya massage ila niliondoka chumbani na nyumbani kwake baada ya mwanaume huyo kutaka kunivua nguo zangu.”

Kufuatia tukio hilo Lupita  ilitishiwa na Weinstein, kuharibia taaluma yake ya uigizaji ila baada ya ushindi wa tuzo ya Oscar 2014, Weinstein alimfuta  muigizaji huyo na kumuomba wafanye filamu ila mrembo huyo alichomoa dili hilo.

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

chrissy-teigen-john-legend-selfie-getty

John Legend na mkewe Chrissy Teigen wanatarajia mtoto wapili

sadockNovember 22, 2017
huhuu

Tiwa savage: Mimi sio mjamzito, hizo ni taarifa za uongo

sadockNovember 22, 2017
clo1

Mkuu wa mkoa, Paul Makonda atembelea ofisi za Clouds Media Group kutoa pole

sadockNovember 22, 2017
pink-beautiful-trauma-tracklist

New Video: P!nk – Beautiful Trauma

sadockNovember 22, 2017