Hot Below Trending

Mafuriko Sierra Leone: Watu 600 watoweka kufuatia maporomoko

Mafuriko Sierra Leone: Watu 600 watoweka kufuatia maporomoko
Profile photo of sadock

Takriban watu 600 wametoweka kufuatia maporomoko ya matope na mafuriko yaliofanya uharibifu mkubwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Freetown nchini Sierra Leone kulingana na msemamji wa rais.

Rais Ernest Bai Koroma awali aliomba usaidizi wa dharura akisema jamii nzima ilikuwa imeangamia.

Takriban watu 400 wamethibitishwa kufariki baada ya maporomoko ya matope katika eneo la Regent na mafuriko katika maeneo mengine mjini Freertown siku ya Jumatatu.

Shjrika la msalaba mwekundu limeonya kuwa hakuna muda wa kutosha kuweza kuwaokoa manusura.Mazishi ya pamoja ya waathiriwa yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano ili kupunguza idadu ya wafu katika chumba cha kuhifadhia maiti.

_97400913_3a7adc6f-7202-41ab-a418-6bd9ad5a4840

Msemaji wa rais Abdulai Baraytay aliambia BBC kwamba miili ilikuwa ikitolewa katika matope hayoi na vifusi.

Jamii nzima inaomboleza.

”Wapendwa wengine wametoweka , takriban zaidi ya watu 600” , alisema.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa kwamba wafanyikazi wake nchini Sierra Leone wamekuwa wakisaidia katika juhudi za kuwaokoa manusura.

”Mikakati inawekwa kuzuia mlipuko wowote wa magonjwa yanayosababishwa na maji kama vile kipindupindu , homa ya manjano na kuharisha”, alisema msemaji wa UN Stephane Dujarric.

Nyumba za jamii zilizokuwa zikiishi juu ya mlima ziliangamia baada ya upande mmoja wa mlima wa Sugar Loaf kuporomoka kufuatia mvua kubwa mapema siku ya Jumatatu.

Waathiriwa wengi walikuwa wakilala wakati wa mkasa huo.

Rais Koroma alizuia machozi alipotembelea eneo la Regent siku ya Jumatatu na kusema kuwa uharibifu huo umepita kiasi.

”Jamii nzima imeangamia tunahitaji msaada wa dharura”, alisema.

BBC Swahili

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017