Pick of the day

Mahakama ya rufaa ya piga chini sheria ya uhamiaji ya Trump

Mahakama ya rufaa ya piga chini sheria ya uhamiaji ya Trump
Profile photo of sadock

Mahakama ya Rufaa nchini Marekani imekataa kuirudisha tena marufuku iliyowekwa na Rais Donald Trump ya wasafiri kutoka nchi saba za kiislamu na Wakimbizi wote kuingia nchini humo.

Jopo la Majaji watatu kwa kauli moja limekataa kuupindua uamuzi uliotolewa na Jaji kutoka mji wa Seattle, ambaye wiki iliyopita alizizuia sehemu za amri iliyotolewa na Rais huyo wa Marekani.

Habari zinasema kwamba uamuzi huo kwa sasa utapelekwa katika Mahakama ya juu.

Na muda mfupi tu baada ya Uamuzi huo wa mahakama kutangazwa, Rais Donald Trum aliwaambia waandishi wa habari kwamba ana uhakika mwisho wake ataibuka mshindi.

Katika hatua nyingine tena Rais Trump ametangaza mfululizo wa amri za Rais kwa lengo la kupunguza uhalifu. Akizungumza wakati wav kuapishwa kwa Mwanasheria mkuu wa nchi hiyo, Rais wa Marekani amesema uhalifu umeongezeka nchini Marekani na utawala wake utalishughulikia suala hilo kuamzia sasa.

Amri hizo zilizotangazwa ni pamoja na kukabiliana na magenge ya madawa ya kulevya na wafanyabiashara za kihalifu.

Comments

comments

Pick of the day

More in Pick of the day

_93798290_79a4dfcf-8f2c-42cd-941c-53bd86b36e27

Wanamgambo wa kundi la Al Shabab wamevamia kambi ya jeshi la Kenya, Somalia

sadockJanuary 27, 2017
U.S. Vice President Joe Biden (R) wipes his eye after President Barack Obama presented him the Presidential Medal of Freedom in the State Dining Room of the White House in Washington, U.S., January 12, 2017. REUTERS/Yuri Gripas

Rais Obama am’suprise makamu wake Joe Biden na Medali ya Rais ya Uhuru

sadockJanuary 13, 2017
MALIA

Video: Obama atoa Hotuba yake ya mwisho kama Rais wa Marekani

sadockJanuary 11, 2017
donald-trump

Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu Marekani

sadockJanuary 10, 2017