Business

Majiji 10 Yanayovutia Kuishi Afrika

Majiji 10 Yanayovutia Kuishi Afrika
Profile photo of sadock
cape-town

Cape Town South Africa

1. Cape Town ni moja ya miji mizuri sana inayovutia duniani, tayari umeshashinda tuzo ya mji unaovutia kutembelea, ni mahali ambapo watu wa Afrika Kusini wanaoishi nje ya Cape Town wanatamani wangekuwa wanaishi hapo, ni mjii ambao ni mzuri kwa kutulia, upo katikati ya milima ya na bahari, embu fikiria jinsi palivyo pazuri, miezi ya kiangazi ni Oktoba – April miezi inayopendwa sana, watu wanapenda kuuita mji huu “Windy City”.

Accra

2. Zaidi ya kuwa mji mzuri, asilimi 20 ya iadadi ya watu wa Ghana milioni 20 wanaishi Accra, Accra umekuwa mji wa kulia bata kwa Wanigeria wengi ni dakika 45 tu kwa ndege kutoka Nigeria mpaka Accra kwa mara nyingi wikiendi Wanigeria husafari hadi Accra kuenjoy, ni mji ambao umejaa migahawa ya kutosha, bars, nightclubs, na shopping malls zimezidi kuongezeka, kuna sehemu nyingi za kitajiri, sehemu ambayo watu wengi inajulikana kama OSU “Oxford Street” watu wanaenda kujiachia nini na vitu kama hivyo.
Hali ya hewa ya Accra ni nzuri pia, wengi waliokwenda ulaya wanarudi nyumbani kutokana na mazingira ya Accra, kuna vyuo vikuu vya kutosha, na serikali imeamua kuinvest katika kuendeleza miundo mbinu na huduma nzuri za kijamii, haya yanamfanya mtu aone Accra utakuwa mji mzuri zaidi ya hapo ulipofikia sasa.

nairobi13. Nairobi kwa haraka unakuwa jiji la Afrika kwa kuwa chaguo la makampuni mengi yakitarajia kuanzisha huduma zao katika jiji hili, Nairobi ni jiji bora kabisa Afrika, General Electric and Rockefeller Foundation hivi karibuni iliuchagua mji wa Nairobi kuwa mwenyeji wa huduma kwa Afrika, pia CCTV ya China news broadcaster. Kuna nyumba nyingi ambazo ni za bei nafuu ukilinganisha na majiji mengine ya Afrika, pia kuna ardhi kubwa.
Zimejengwa apartments nyingi sana, zikiwa na mabwawa ya kuogelea na sehemu za kufanyia mazoezi.
Ni vizuri ukiwa na usafiri wako, lakini unaweza ukatumia tax, matatu na boda boda ambazo ndo zinatumika sana na watu wa kawaida kwa sababu ya foleni kubwa mjini.

johannesburg1

Johannesburg

4.Kuanzia dakika uliyoshuka kutoka kwenye ndege kwenye airpot ya OR Tambo Internationa, unakubali kwanini Johanesburg inatajwa kama jiji bora, uwanja wa ORTIA unashindana na viwanja vya nchi zilizoendelea, ni wakisasa, mkubwa na zinapatikana karibu kila huduma yakiwemo maduka ya vitu mbalimbali, migahawa, kama maeneo mengine ya Afrika Kusini na kuwa mji wa kibishara Afrika.
Toka 1800 maelfu ya wageni walikwenda katika jiji hilo kwa ajili ya kutafuta ajira katika machimbo ya madini. Watu wanazidi kukumiminika kutoka sehemu nyingine nje ya Johannesburg na nje ya Afrika Kusini yenyewe, kwa ajili ya kutengeneza mkwanja na kupata kazi pia.
Johannesburg pia inavutia makampuni mengi ya Kiafrika kwa sababu zinakuwa zikipatikana fursa za Kimataifa, hivi karibuni kumekuwa na juhudi za kufufua sehemu za ndani ya jiji hilo zilozokuwa zimetelekezwa. Pesa zimetolewa kwa serikali za mitaa kwa ajili ya kusafisha mitaa na kurepea majengo ya zamani.
Kuna apartments mpya nyingi ambazo zinapendezesha jiji hilo sana, kuma shopping malls za kuvutia, ukitoa mall kubwa ya Sandton City na Eastgate, utashangazwa na ukijani uliozunguka jiji hilo, Johannesburg inajulikana kuna msitu mkubwa duniani ambao umetengenezwa na mkono.

gaborone-capital-of-botswana

5. Ikiwa ni jiji changa, ilipata uhuru wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1960, Gaborone imeendelea kustawi vyema, siasa zilizokomaa na uchumi imara, mji mkuu wa Botswana Gaborone unatajwa kuwa mji wa amani, ina eneo dogo sana na watu zaidi 230,000, lakini kuna watu wa mataifa mbalimbali na sehemu nyingi ambazo ungependa kuziona.
Gabs kama watoto wa town wanavyouita unajulikana kwa kutengeneza rough diamond, almasi hiyo inaasilimia kubwa sana za kuutengeneza mji huo kupitia pesa inayopataikana, nje ya ya uchumi wake kusaidiwa na uchimbaji wa almasi pia ni sehemu ambayo inasafirisha nyama ya ng’ombe nchi za ulaya na kukuwa kwa utalii.
Viwanja vya michezo vya kisasa, ilishuhudiwa wakiwa wenyeji wa Africa Junior Athletic Championship mwaka 2011 na imeleta ushindani mkubwa kwenye kutaka kuwa mwenyeji wa African Youth Games 2014.
Pia Gaborone imeungana na mji mkuu wa Afrika kusini Pretoria, inafanana sana jirani yake Pretoria inagawa Gaborone ni salama zaidi.

Libreville Gabon

Libreville Gabon

6. Mji unaopendeza na wa kisasa, ni jiji kubwa ambalo sehemu yake kubwa ni nyumba za kuishi wananchi wake, watu wengi hapa ni vijana, nusu ni miaka 19 na chini ya hapo na wanaishi mjini. Watu wanaoandikishwa mashuleni Gabon ni zaidi ya asilimia 70 na watu waliosoma inaenda karibia asilimia 90. Ndani ya Libreville ni zaidi ya asilimia 63, ambao wanafanya kazi kwenye migahawa, hoteli, na maduka.
Kutokana na kutaliwa na Ufaransa, lugha ya Kifaransa imekuwa lugha yao rasmi, ni mji ambao una majengo ya kuvutia yaliyojengwa makandarasi wenye sifa,. Jiji hili lipo pembezoni mwa ufukwe wa bahari kitu ambacho kinafanya kutoka kazini na kwenda kupunga upepo kuwa rahisi.

Ulijengwa uwanja mpya wa mpira ambao ulitumika kwenye fainali za kombe la mataifa ya Afrika 2012, maandalizi ya michuano hiyo ilishuhudia serikali ya nchi hiyo ikiwekeza kwenye kutengeneza barabarabara na sehemu nyingine ambazo zinatumiwa na wananchi.
Mafuta ndiyo kimbilio lao kubwa ambalo linasaidia uchumi kukuwa pamoja na sehemu za uchimbaji wa madini, ukiwa mbali na sehemu za kuchimbia madini unavutiwa na milima yenye uoto wa asili, Serikali ya nchi hiyo miaka 10 iliyopita ilihakikisha inatenga eneo la asilimia 10 la nchi hiyo kuwa hifadhi ya taifa inayoitwa Akanda, ambapo imefanya nchi hiyo kujulikana kwa watalii kutembelea nchi hiyo.

 

tunis7. Tunis mjii mkuu wa Tunisia unakamata namba 7, Tunisia ilitajwa kama sehemu ya pili yenye furaha (baada ya Algeria) ukiwa ni mji wenye mali nyingi katika majiji ya dunia ya Kiislamu, mji mkuu wa Tunisia unatajwa ni mji wenye gharama sana kuishi kwa wageni, ukiwa Tunis, kutembea sehemu mbalimbali ni kwa kutumia reli ambayo inaunganisha viunga vya mji huo na sehemu nyingine za nchi. Tunisia ilitawaliwa na Wafaransa kwa zaidi ya miaka 70, Tunisia kuna utajiri wa utamaduni.
Pia watu wake wanaishi miaka mingi inakadiriwa kufikia miaka 74.6, watu wa Tuniasia wanafuraha, na inaaminika furaha ikiwemo katika maisha hata mtu huishi miaka mingi zaidi.

 

dar-es-salaam

8. Jiji la Dar es salaam Tanzani linakamata nafasi ya 8, Dar es salaam ni jiji linalokuwa kwa kasi, kuanzia miundo mbinu kwa ajili ya watu wanaoishi hapo, idadi ya wakazi wake inaongeza kwa zaidi ya asilimia 3 kila mwaka, ni mji wa tatu unakuwa kwa haraka Afrika, na watatu duniani.
Pia ni mji ambao unawageni wengi ingawa Dar es salaam sio mji mkuu tena, lakini Dar es salaam ndiyo jiji kubwa nchini Tanzania, na umebaki kuwa kitovu cha uchumi na siasa. Kumekuwa na uwekezaji mkubwa katika elimu, ambapo elimu ya msingi inapatikana bure, kitu ambacho kilipigiwa kelele na Organization za kimataifa kuongeza idadi ya kuandikisha wanafunzi hadi kufikia zaidi ya asilimia 90.
Dar es salaam pia panatakina vyuo vikubwa vya serikali na binafsi, Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambacho hivi karibuni kilisherekea miaka 50 toka kuanzishwa na idadi ya wanafunzi wanaoingia chuoni hapo imeongezeka.
Kuna chuo Teknolojia kinachoitwa (DIT) Dar es salaam Institute of Technology, chuo kinachoongoza katika kutoa mafunzo ya kiufundi jijini hapo. Reli zilizokuwa hazitumikia zimefufuliwa kwa ajili ya usafiri jijini hapo,.
Milioni za pesa zimetumika kutengeza barabara za jiji, kufanya usafiri kuwa mzuri, Dar es salaam inapata vipindi vya joto la wastani, baridi kidogo kitu kinachofanya jiji hilo kuvutia watu wengi zaidi kuishi ikiwemo shughuli za kiuchumi kwa kufanyika biashara mbalimbali.
Dar es salaam imebarikiwa ufukwe mzuri ambao umezungukwa na migahawa mizuri, mahoteli, pia ikiwemo kisiwa cha Zanzibar, na kivuko kifupi cha kwenda Kigamboni.
Shopping malls kubwa, ikiwemo Mlimani City na nyingine na nightsclub nyingi na sehemu nyingi za kuvutia.

windhoek

9. Windhoek mji mkuu wa Namibia unashikilia nafasi ya 9, Kuanzia kwenye lugha mpaka jinsi majengo yake yanavyoonekana, utajua kabisa Mjerumani alihusika na kushawishi mji huo uwe hivi, ikikumbusha mtawala wa mwisho wa Namibia alikuwa Mjerumani. Usitegemee kuwa na idadi ya watu wengi, kuna idadi ya watu 320,000. Ni mji mdogo lakini ni sehemu inayovutia taasisi nyingi za serikali kuwepo hapo, unafanya uwe mji wa kisiasa, kitamaduni, jamii na uchumi.
Namibia inajulikana zaidi kwa jangwa linaloitwa Namib, ikiwa ni la zamani sana duniani, pia Windhoek inajulikana kwa bia yake. Windhoek Lager ni moja ya bia inayokuwa kwa haraka mjini hapo na inauzwa zaidi ya nchi 20 duniani.
Kinywaji hicho cha zamani zaidi bado kipo imara kikiwa na sifa yake ile ile ya kupendwa, ikiwa ndio biashara kubwa katika jiji hilo na kwa sasa ina migahawa yake, bars na shots.
Ukitembelea hapo na sehemu nyingine za jiji hilo, tegemea kukutana na watu wa tofauti tofauti wenye historia mbalimbali, wakiwa ni wazawa wa San, Hereo, na kundi la Kavango.
Mji huo unavutia kwa vitu vingi, kwanza ni mji msafi sana, usalama mkubwa, kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine ni rahisi, zote kwa tax na mabasi, wanatoa huduma nzuri ya usafri na inasaidia kwa sababu barabara pia zinawekwa katika hali nzuri.

Kigali10. Kigali Rwanda unafunga top 10 ya majiji yanayovutia kuishi Afrika, Kigali Rwanda unafunga top 10 ya majiji yanayovutia kuishi Afrika, Kuanzia kwenye upanukaji wake wa baishara za ndani, mpaka kwenye utengenezaji wa barabara inasaidia kuondoa foleni kabisa, Kigali taratibu unakuwa moja ya miji inayokuwa kwa kasi kwenye bara la Afrika.
Kigali ipo katikati ya Rwanda, Kigali ni sehemu inayoishi watu karibia milioni moja na na pia kuna jumuiya watu wengi wageni waliopo Rwanda ambao wanafurahia mambo tofauti tofauti yanayopatikana Kigali.
Kama nchi nyingi za Afrika, kuna sehemu mbili za kuishi, ikiwa watu wake wengi wanaishi sehemu za vijijini, miundo mbinu ya kisasa inaendelea kujengwa katika kitovu cha biashara, Maendeleo makubwa Rwanda ni Kigali Tower, jingo lenye ghorofa 20 lenye maduka ya wafanyabiashara, hilo ndilo jingo refu la jiji hilo la Kigali.
Kuishi Kigali ni gharama, ikisababishwa na bidhaa nyingi zinazotoka nje ya Rwanda, inasababisha bei iwe juu, kikubwa kwenye uchumi wa Rwanda imebaki ni parks za wanyama, kikubwa ikiwa ni gorilla wanaopatikana milimani.
Utalii unabaki ndio muhimu cha kipato cha nchi cha kuingiza pesa za kigeni, ongezeko hilo imeshuhudia uwekezaji mkubwa katika hoteli, huduma na kampuni nyingi za kitalii.

Comments

comments

Business

More in Business

t4

#TecnoDude Ya Washa dude kitaani

sancho songJuly 10, 2017
tecno1

TECNO YAAMSHA DUDE KWA BEI CHEE

sancho songJuly 6, 2017
t

Tecno Dude Mkombozi Wa Watanzani.

sancho songJuly 4, 2017
sta

List ya mastaa wa soka barani Ulaya kuja Tanzania yazidi kuongezeka

sancho songJune 20, 2017