Hot Below Trending

Man United yachezea 2-1 kwa Man City

Man United yachezea 2-1 kwa Man City
Profile photo of sadock

Manchester City imeendeleza ubabe wake kwenye ligi kuu soka ya England baada ya kumchapa hasimu wake wa jiji moja Manchester United 2-1.

Katika mchezo huo ambao City ilimiliki mpira wakati mwingi, ilipata goli lake la kwanza kupitia David Silva dakika ya 43 kabla ya Marcus Rashford kusawazisha dakika ya 45 na Nicolás Otamendi kupachika la pili na la ushindi dakika ya 54.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kwa sasa ni wazi asilimia kuwa ya ubingwa msimu huu ikaenda kwa City.

Nusura Lukaku asawazishe matokeo dakika za mwisho wa mchezo kabla ya mlinda mlango wa City Ederson kuokoa

”Wamecheza vizuri, wengi walitarajia hili, ni vigumu kuwakabili kama hauna timu imara zaidi yao, tumemkosa Pogba ambaye angeweza kuleta madhara kwao, nafikiri wanaweza kuwa mabingwa msimu huu,” alisema Mourinho.

Meneja wa City Pep Guardiola ameisifu timu yake kwa kucheza kama Barcelona na kuongeza kuwa vile alivyotoa maelekezo ndivyo walivyofanya.

City ambao wamepoteza alama mbili tu katika michezo 16 wanasalia kileleni wakiwa na alama 46 , huku United ikiwa na alama 35.

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017