Entertainment

Mbali ya Pusha T, hawa ni rappers wengine waliowahi kushika nafasi za juu kwenye label za music

Mbali ya Pusha T, hawa ni rappers wengine waliowahi kushika nafasi za juu kwenye label za music
Profile photo of sadock

Siku ya jana taarifa za kuwa rapper Push T ameteuliwa na Kanye west kuwa raisi wa label ya G.O.O.D. Music ziliwekwa wazi, tumekutafutia orodha ya rappers wengine wakubwa waliowahi kushika nafasi za juu kwenye label kubwa za muziki

Jay Z

Jina lake halisi ni Shawn Corey Carter amewahi kuwa raisi wa label ya Def Jam kwa muda wa miaka minne kuanzia mwaka 2004 hadi 2007, kipindi cha uongozi wake aliibua vipaji vya wasanii waliokuja kufanya vizuri ikiwemo Rihanna na Ne-yo. Aliachana na Def Jam ili aweze kuanzisha label yake mwenyewe Roc Nation.

 

DJ khaled 

Khaled Mohamed Khaled aka Dj Khaled amewahi kuwa raisi wa Def Jam south mwaka 2009, kipindi cha uongozi wake alisimamia kazi za wasanii wakubwa ikiwemo Rick Ross, Young Jeezy, Ludacris na Ace Hood.

 

Scarface

Huyu alipokea uongozi mwaka 2010 baada ya Dj Khaled, wakati wa uongozi wake, def jam iliachia album nyingi zilizofanya vizuri sokoni ikiwemo ‘Loud’ ya Rihanna, ‘My Beautiful Dark Twisted Fantasy‘ ya Kanye west, ‘Libra Scale‘ ya Neyo,  ‘Distant Relatives‘ ya Nas na Damian marley na nyingine.

Jermaine Dupri

Huyu alikua raisi wa label mbili za muziki Virgin records aliyoteuliwa mwaka 2005 na Islands records aliyoteuliwa kuwa raisi mwaka 2007, Jermaine Dupri ndio aliyegundua kipaji cha Bow wow.

Snoop Doog

Calvin Cordozar Broadus, Jr aka Uncle snoop mwaka 2009 alitajwa kuwa mwenyekiti wa EMI priority records iliyowahi kusimamiza kazi za wasanii wa NWA, baada ya Snoop kuchaguliwa iliachia album ya kumi iliyowashirikisha wasanii kama  Teddy Riley, Nottz, The Neptunes, The-Dream, and Terrace Martin. pamoja na R. Kelly, Soulja Boy Tell ‘Em, na Brandy.

 

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

mgid_ao_image_logotv

New Video: Jennifer Hudson – Burden Down [Official Music Video]

sadockDecember 13, 2017
_99171871_cef98067-831f-46ed-9b08-b20ac967d873

Oscar Pistorius apata majeraha baada kupigana gerezani

sadockDecember 13, 2017
eminem-e1507948158888-825x620

Eminem: Huwa narekodi ngoma zaidi ya 50 ili nipate ngoma 20 bora kwa ajili ya Album

sadockDecember 11, 2017
WAKADR

Waka ya Diamond yashiKa namba 1 Tanzania, Kenya na Uganda kwenye mtandao wa YouTube

sadockDecember 11, 2017