Hot Below Trending

Mchezaji wa mpira wa miguu, Indonesia afariki dunia uwanjani

Mchezaji wa mpira wa miguu, Indonesia afariki dunia uwanjani
Profile photo of sadock

Mlinda mlango wa klabu ya ligi kuu ya Indonesia amefariki baada ya kugongana na mchezaji mwenzake uwanjani.

Choirul Huda, mwenye miaka 38, alikimbizwa hospitalini siku ya Jumapili lakini muda mfupi baadae ilitangazwa kwamba amefariki dunia.

Katika taarifa iliyotolewa na tovuti ya klabu yake Persela FC , daktari wa timu Yudistiro Andri Nugroho amesema mchezaji huyo alifariki baada ya kupata madhara makubwa kifuani.

Anasema mgongano huo ulisababisha kushindwa kupumua kwa Huda.

Ameongeza kuwa madaktari walijaribu kuokoa maisha yake bila mafanikio.

Mchezo huo uliisha kwa Persela kuifunga Semen Padang 2-0.

Maelfu ya mashabiki wamefika hospitalini alipofia mchezaji huyo aliyecheza michezo 500 ya ligi kuu kwa klabu yake pekee.

 

BBC Swahili

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

chrissy-teigen-john-legend-selfie-getty

John Legend na mkewe Chrissy Teigen wanatarajia mtoto wapili

sadockNovember 22, 2017
huhuu

Tiwa savage: Mimi sio mjamzito, hizo ni taarifa za uongo

sadockNovember 22, 2017
clo1

Mkuu wa mkoa, Paul Makonda atembelea ofisi za Clouds Media Group kutoa pole

sadockNovember 22, 2017
pink-beautiful-trauma-tracklist

New Video: P!nk – Beautiful Trauma

sadockNovember 22, 2017