Entertainment

Mkubwa Fella – Alikiba ni mwanangu wa dhahabu

Mkubwa Fella – Alikiba ni mwanangu wa dhahabu
Profile photo of sadock

Meneja Mkubwa Fella ambaye pia ni mingoni mwa wale wanaomsimamia Diamond Platnumz amesema hilo haliwezi kumzuia kufanya kazi na Alikiba.

Kutokana na ukaribu wake na Diamond mashabiki wengi wamekuwa wakidhani kuwa yeye ni team Diamond, hata hivyo ameeleza katika kazi hakuna utimu.

“Kwanza ukae ukijua sijawahi kusema sifanyi kazi na mtu yeyote, Alikiba mimi ni mwanangu wa dhahabu, ni mwanangu wa gold wala wala usiseme kuna hiki na hiki japokuwa wanasema chawa, basi chawa waje vizuri kwa sababu mimi ndiye meneja wa kwanza katika muziki huu sina pingamizi kusema nitafanya kazi na mtu niogope kufanya kazi na mtu,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.

“Wote ni wanangu mimi ni mkubwa na wanae, kwa hiyo Alikiba ni mwanangu, haijawahi kuonekana hata siku moja mimi na Alikba tunagombana,” amesema Fella.

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

22637347_151631285443331_1675299238445056000_n

Picha: Rapper Gucci Mane afunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Keyshia Ka’oir

sadockOctober 18, 2017
luluuuu

Kesi ya mauaji bila kukusudia inayomkabili Elizabeth Lulu kuanza kusikilizwa wiki hii

sadockOctober 17, 2017
_98330961_4a22e640-0e79-444e-abc9-f7cb171064d0

Ed Sheeran apata ajali ya baiskeli, avunjika mkono

sadockOctober 17, 2017
maxresdefault (8)

Aslay: Huwezi nifananaisha na Diamond na Alikiba, nitajitahidi kuwafikia

sadockOctober 17, 2017