Entertainment

Mkuu wa mkoa, Paul Makonda atembelea ofisi za Clouds Media Group kutoa pole

Mkuu wa mkoa, Paul Makonda atembelea ofisi za Clouds Media Group kutoa pole
Profile photo of sadock


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Paul Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Dar es salaam mapema leo ametembelea Ofisi za Clouds Media Group kutoa pole ikiwa ni siku moja baada ya Ofisi hizo kukumbwa na janga la moto.

Mhe. Makonda amefika Ofisini hapo kutoa pole kwa janga la moto lililoipata Ofisi hiyo siku ya jana majira ya saa nne asubuhi kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dar es salaam.

Viongozi wengine wa serikali waliofika Ofisini hapo ni Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni, Ally Hapi na Meya wa Manspaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta.

Hata hivyo, Tayari matangazo ya vituo vya Clouds FM na Clouds TV vimerejea hewani baada ya kupotea siku nzima ya jana kutokana na hitilafu iliyosababishwa na moto huo ambao chanzo chake hadi sasa hakijajulikana.

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

mgid_ao_image_logotv

New Video: Jennifer Hudson – Burden Down [Official Music Video]

sadockDecember 13, 2017
_99171871_cef98067-831f-46ed-9b08-b20ac967d873

Oscar Pistorius apata majeraha baada kupigana gerezani

sadockDecember 13, 2017
eminem-e1507948158888-825x620

Eminem: Huwa narekodi ngoma zaidi ya 50 ili nipate ngoma 20 bora kwa ajili ya Album

sadockDecember 11, 2017
WAKADR

Waka ya Diamond yashiKa namba 1 Tanzania, Kenya na Uganda kwenye mtandao wa YouTube

sadockDecember 11, 2017