Hot Below Trending

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani
Profile photo of sadock

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ameorodheshwa kuwa wa tatu miongoni mwa wachezaji wa thamani ya juu zaidi duniani, kwa mujibu wa utafiti mpya.

Utafiti huo wa shirika la takwimu za michezo la CIES unasema Kane thamani yake ni euro 194.7m (£172.65m).

Wanaomzidi ni mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 25, na mwenzake wa Barcelona Lionel Messi, 30, pekee.

Mshambuliaji huyo wa England mwenye miaka 24, alifungia klabu na taifa mabao 56 mwaka jana, na kumfanya mfungaji mabao bora zaidi Ulaya.

Mwenzake wa Spurs na England Dele Alli, 21, yumo nafasi ya sita oordha hiyo na ndiye wa pili orodha hiyo kwa wachezaji walio Ligi ya Premia.

Makadirio ya bei ya uhamisho ya wachezaji ya CIES (euro)
1. Neymar (PSG) – 213m 6. Dele Alli (Tottenham) – 171.3m
2. Lionel Messi (Barcelona) – 202.2m 7. Kevin de Bruyne (Man City) – 167.8m
3. Harry Kane (Tottenham) – 194.7m 8. Romelu Lukaku (Man Utd) – 164.8m
4. Kylian Mbappe (PSG) – 192.5m 9. Antoine Griezmann (Atletico Madrid) – 150.2m
5. Paulo Dybala (Juventus) – 174.6m 10. Paul Pogba (Man Utd) – 147.5m

CIES walitumia umri, nafasi anayocheza mchezaji, muda wa mkataba wake, uchezaji wake uwanjani na hadhi yake kimataifa kufanya makadirio hayo ya thamani.

Kiungo wa Manchester City Kevin de Bruyne, 26, fowadi wa Manchester United Romelu Lukaku na kiungo wa kati Paul Pogba, wote wa miaka 24, ndio wachezaji wengine wanaocheza England walio kwenye 10 bora.

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, aliyetawazwa mchezaji bora zaidi wa kiume duniani na Fifa 2017 yumo nafasi ya 49 kwenye orodha hiyo.

Thamani yake ni euro 80.4m (£71.29m)

Mchezaji mpya wa Barcelona Philippe Coutinho, 25, amewekwa nafasi ya 16 ,thamani yake ikikadiriwa kuwa £33m chini ya bei ambayo Barca walilipa Liverpool kumchukua.

Kipa wa thamani ya juu zaidi ni Marc-Andre ter Stegen, 25, wa Barcelona ambaye thamani yake ni euro 96m (£85.13m) na Samuel Umtiti, 24, ndiye beki ghali zaidi, thamani yake ikiwa euro 101m (£89.56m).

Paulo Dybala, 24, wa Juventus ndiye wa thamani ya juu zaidi Serie A thamani yake ikiwa £155.18m naye Robert Lewandowski, 29, wa Bayern Munich anaongoza kwa wachezaji wa Bundesliga (£94.88m).

wachezaji wengine wa Ligi ya Premia walio kwenye 30 bora
11. Leroy Sane (Man City ) – 140.6m 20. Alvaro Morata (Chelsea) – 108m
12. Mohammed Salah (Liverpool) – 140.5m 23. Roberto Firmino (Liverpool) 102.9m
13. Raheem Sterling (Man City) – 138.2m 27. Bernardo Silva (Man City) – 98.8m
15. Marcus Rashford (Man Utd) – 126.8m 28. Sergio Aguero (Man City) – 98.7m
17. Gabriel Jesus (Man City) – 122.6m 29. Christian Eriksen (Tottenham) – 98.4m
18. Eden Hazard (Chelsea) – 119.6m 30. Alexandre Lacazette (Arsenal) – 97.6m

 

 

BBC Swahili

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017
Vanessa Mdee

Vanessa Mdee asaini mkataba mnono na Universal Music Group, kusimamia usambazaji wa kazi zake nje

sadockDecember 20, 2017