Entertainment

Peter Crouch aingia Guinness World Records kwa kufunga mabao mengi ya kichwa

Peter Crouch aingia Guinness World Records kwa kufunga mabao mengi ya kichwa
Profile photo of sadock

Mshambuliaji wa klabu ya Stoke ya England Peter Crouch ameingizwa kwenye kitambu cha rekodi za dunia cha Guinness World Records cha mwaka 2018 kwa kufunga mabao mengi zaidi kwa kichwa Ligi ya Premia.

Crouch amefunga mabao 51 kwa kichwa katika ligi hiyo, mabao matano zaidi ya mchezaji wa zamani wa Blackburn na Newcastle Alan Shearer.

_98236555_crouch-main

Crouch, 36, kwa jumla amefunga mabao 105 Ligi Kuu ya England katika mechi 436 alizochezea jumla ya klabu sita ligi hiyo.

“Iwapo wewe ni mshambuliaji wa kati, unafaa kuwa eneo la hatari, tayari kufunga bao kwa kichwa,” amesema Crouch.

“Hivi ndivyo nimekuwa nikicheza na hilo sitawahi kulibadilisha. Washambuliaji wa kati wakaokaa nje ya eneo la hatari hunishangaza sana, siwezi kuelewa huwa wanafikiria nini.”

Crouch alifunga bao la ushindi mechi ya karibuni zaidi ya Stoke walipocheza dhidi ya Southampton.

 

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

mgid_ao_image_logotv

New Video: Jennifer Hudson – Burden Down [Official Music Video]

sadockDecember 13, 2017
_99171871_cef98067-831f-46ed-9b08-b20ac967d873

Oscar Pistorius apata majeraha baada kupigana gerezani

sadockDecember 13, 2017
eminem-e1507948158888-825x620

Eminem: Huwa narekodi ngoma zaidi ya 50 ili nipate ngoma 20 bora kwa ajili ya Album

sadockDecember 11, 2017
WAKADR

Waka ya Diamond yashiKa namba 1 Tanzania, Kenya na Uganda kwenye mtandao wa YouTube

sadockDecember 11, 2017