Entertainment

Picha: Serena Williams afunga ndoa, Mastaa wamwagika kwenye harusi yake

Picha: Serena Williams afunga ndoa, Mastaa wamwagika kwenye harusi yake
Profile photo of sadock

Mchezaji tenis raia wa Marekani mwanadada, Serena Williams hapo jana siku ya Alhamisi amefanikiwa kufunga ndoa na mumewe Alexis Ohanian huko Contemporary Arts Center, New Orleans nchini Marekani.

Williams mwenye umri wa miaka 36 na mumewe Alexis Ohanian 34 walitangaza juu ya ndoa yao toka mwezi Desemba mwaka 2016 wakati sherehe ya uchumba wao ikinogeshwa na ujio wa mtoto wao wakike  Alexis Olympia Ohanian ikiwa ni miaka miwili tu tangu kuanza kwa mahusiano yao mwaka 2015.

Ndoa hiyo ambayo haikuwa wazi ili hudhuriwa na watu wakaribu na familia hiyo, marafiki pamoja na mtoto wao wakike mwenye umri wa miezi miwili, Alexis Olympia Ohanian Jr.

Ohanian, ambaye ni muanzilishi wa mitandao ya habari za kijamii na tovuti ijulikanayo kama ‘Reddit’ na Williams mchezaji bora wa tenis duniani, harusi yao iliyofungwa eneo la Contemporary Arts Center imehudhuriwa na marafiki wakaribu akiwemo dada yake, Venus Williams,Beyonce, Kim Kardashian, Ciara Lala, Kelly Rowland, Eve Longoria akiwa na mumewe Jose Baston, pamoja na mchezaji tenis Caroline Wozniacki akiwa na mpenzi wake mchezaji wa NBA, David Lee.

Kim Kardashian akiwasili katika ndoa hiyo akiwa amevalia kivazi cheusi   

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017
Vanessa Mdee

Vanessa Mdee asaini mkataba mnono na Universal Music Group, kusimamia usambazaji wa kazi zake nje

sadockDecember 20, 2017