Lifestyle

Polisi Kagera amtaja muhusika mkuu anayehusika na uchomaji wa nyumba za watu

Polisi Kagera amtaja muhusika mkuu anayehusika na uchomaji wa nyumba za watu
Profile photo of sancho song

Kutokana na kuwepo kwa matukio ya nyumba za watu kuungua moto Jeshi la Polisi Kagera limewakamata watu wawili wanaosadikiwa kuchoma moto nyumba za watu katika kijiji cha Bugasha kilichopo Kata ya Mayondwe, Muleba..

Kamanda wa Polisi Kagera Augustine Ollomi amesema kuwa July 2 mwaka huu ilichomwa moto nyumba nyingine ya mzee wa miaka 60 na kufikisha jumla ya nyumba 14 tangu zimeanza kuchomwa mpaka sasa.

Kamanda Ollom amewataja waliokamatwa kuwa ni Badiru Daniel miaka 32 aliyejitambulisha kuwa ni Mshubi lakini Jeshi la Polisi limembaini kuwa ni Mrundi, na wa pili ni Angela Karisti miaka 36 Mhaya mkazi wa kijiji Bisole kata mhutwe ndani ya wilaya hiyo.

Polisi wamesema hadi sasa tayari wameshamjua  mhusika mkuu wa matukio hayo ambaye anafahamika kwa jina la Shakiru Mohammed miaka 42 mkazi wa kijiji Bugasha

Comments

comments

Lifestyle

More in Lifestyle

170111_WAR_tillerson.jpg.CROP.promo-xlarge2

Marekani yasema haina uadui na Korea Kaskazini

sadockAugust 2, 2017
kibi

Kibiti Geust House na Viwanja vya panda bei

sancho songJuly 31, 2017
zzzzzzzz

(Eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia),Haya ni baadhi ya yale maneno 68 ya Diamond kwa Zari

sancho songJuly 29, 2017
mazi

Mazishi na muziki -Ghana

sancho songJuly 27, 2017