Hot Below Trending

Polisi watibua jaribio la pili la shambulizi Uhispania

Polisi watibua jaribio la pili la shambulizi Uhispania
Profile photo of sadock

Maafisa wa polisi wa Uhispania wanasema kuwa wamewaua watu watano katika mji wa Cambrils ili kuzuia jaribio la pili la shambulio baada ya shambulio la hapo awali kufanyika mjini Barcelona.

Washambuliaji walikuwa wamevalia vilipuzi , polisi wamesema.

Watu 13 walifariki huku makumi wakijeruhiwa baada ya gari dogo kuingia katika eneo la watu mjini Barcelona eneo la Las Ramblas siku ya alhamisi mchana. Dereva wa gari hilo alitoroka na bado anaswaka.waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy alisema kuwa lilikuwa shambulio la kijihadi.

Mamlaka sasa wanahusishwa shambulio hilo la Barcelona pamoja na lile la Camrils huku mlipuko ukiripotiwa katika nyumba moja siku ya Jumatano jioni katika mji wa Alcanar ambapo mtu mmoja alifariki.

602255-000rn56c

Awali afisa mkuu wa polisi Josep Lluis Trapero alisema kuwa inaonekana wakaazi wa eneo la nyumba ya Alcanar walikuwa wakiandaa kuntengeza kilipuzi .

Mjini Cambrils watu saba akiwemo afisa mmoja wa polisi alijeruhiwa wakati gari lilipovurumishwa katika umati wa watu mapema siku ya Ijumaa kulingana na huduma za dharura huko Catalan.

Mtu mmoja yuko katika hali mahututi.

Vyombo vya habari vya Uhispania viliripoti kwamba washambuliaji waliuawa wakati walipojaribuo kutoroka baada ya gari lao kupinduka.Baadaye misururu ya milipuko ilifuatia.

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017