TEAM TZ


Aliyekuwa mchumba wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, mlimbwende Wema Isaac Sepetu ameivua rasmi pete ya uchumba kufuatia kupigwa chini na msanii huyo Ishu hiyo ya kusikitisha, ilijiri Jumatano ya Oktoba 19 mwaka huu, saa chache baada ya kujiridhisha na taarifa za kuachwa kwake.

Wema aliivua pete hiyo ya dhahabu na kuibwaga sakafuni akiwa ndani ya chumba nambari 35, Hoteli ya Lamada iliyopo Ilala, jijini Dar es Salaam ambako amepiga kambi na wenzake kwa ajili ya kurekodi filamu.

Aidha, baada ya tukio hilo, msanii nyota wa muvi za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliiokota na kuivaa kwenye kidole husika huku akisema ‘anaosha nyota’.

“Hee, ngoja niivae miye nioshee nyota, jamani! Mh,” alisikika akisema Lulu licha ya kwamba wakati huo, Wema alikuwa akibubujikwa machozi.

Mpaka mapaparazi wetu wanaondoka eneo la tukio, Wema alikuwa bado akilia huku akisema anajuta kuvishwa pete na Diamond ambaye amemuacha njia panda.

Alisema katika maisha yake hajawahi kuachwa, Diamond amemfanyia tukio la ajabu sana na haamini masikio yake achilia mbali macho.

Jumapili ya Oktoba 2 mwaka huu, ndani ya Maisha Club, jijini Dar es Salaam, Diamond alimvisha Wema pete ya uchumba tukio ambalo lilishuhudiwa na mashabiki wao kibao.

Oktoba 18 mwaka huu, ndani ya Hoteli ya Lion, Sinza jijini Dar es Salaam, Diamond aliwaambia waandishi wa habari kwamba, ameamua kummwaga Wema kufuatia jaribio lake la kutaka kumtenganisha na mama yake mzazi.

Habari za kuachika kwa Wema, zimeandikwa kwa kina ndani ya gazeti la Risasi Ijumaa la jana. Kwa maana hiyo basi, Wema amedumu na pete katika kipindi cha siku 16 tu.

 

Source : www.globalpublishers.info

Views: 7980

Tags: AVUA, PETE, RASMI, WEMA

Comment

You need to be a member of TEAM TZ to add comments!

Join TEAM TZ

Comment by DEOGRATIUS TESHA on November 16, 2011 at 2:44pm

haina noma walihic kuwa ni fashion!

Comment by ezekiel kaponela on November 16, 2011 at 2:29pm

acheni kuchekesha mbona  mpo south

Comment by Frank venance on November 16, 2011 at 12:17am
Pole dada bt jua ckuzte mteswa uteswa!
Comment by collins mr appletaste fravour on November 14, 2011 at 4:18pm

wote malaya

Comment by frank christin kessy on November 12, 2011 at 8:07pm

mapenzi  kazi

Comment by ahamada othoman on November 11, 2011 at 1:49pm

pole dada likuwa nikuzalilisha tu si kukuvisha pete limbokekitu mshikaji tu.

Comment by ahamada othoman on November 11, 2011 at 1:46pm

sioviruri diamond tatizo ulimbikeni tu wa wanaweke dada wema tulia tu mungu atakulipia utapata mmume mweme.

Comment by harry thabeet chazza on November 10, 2011 at 4:41pm

ckuzote malaya ajui kutulia aya kikwap sasa na sasa atachina dada wa w2 embu jaribu kumuomba msamaha atakusamee mana dimond nae c limbuken 2....!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Comment by http://www.msikecorner.blogspot. on November 9, 2011 at 8:52pm

wote wallikurupuka

 

Comment by charles lyimo on November 9, 2011 at 12:45pm

Nilijua2 ila uyu dada anaitaji maombi tumuombee jamani sio kumsematu

G5 CLICK - LATEST NEWS

EXCLUSIVE - PICHA MPYA ZENYE UTATA ZA DIAMOND PLATNUMZ NA ZARI THE BOSS LADY WAKIWA NDANI YA JIJI LA DAR.

Diamond Platnumz na Zari the boss lady kwa mara ya kwanza walikutana kwenye ndege wakati wakitokea South Africa kuja Tanzania na kupiga picha za kawaida za pamoja ambazo walizi-post kwenye mtandao wa instagram. SASA LEO TEAMTZ.COM…


FREE FLAVA

TOP PHOTOS

1. IMG-20150312-WA0014

Added by Salvatory Miheza on March 14, 2015

3. Nah real

Added by ChuiChui-Teamtz on March 30, 2015

 

© 2015   Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service