TEAM TZ

Ustadhi Yahya Michael, mkazi wa Dar, hivi karibuni amejitokeza na kudai kuwa yeye ndiye mganga aliyempaisha mwanamuziki Nasibu Abdu ‘Diamond Platnumz’ ambaye kwa sasa ni kinara wa Bongo Fleva, Risasi Jumamosi lina mkanda kamili.
MH! SIKU HIZI ANAJIFANYA SUPASTAA
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum maeneo ya Magomeni, Dar, mganga huyo alidai kuwa pamoja na jitihada kubwa alizofanya kumpaisha Diamond lakini anamshangaa kwa kuwa amesahau alikotoka na anajifanya supastaa.
Alidai kuwa siku hizi akimpigia simu, Diamond huwa hapokei, tofauti na zamani alipokuwa akihangaika kuchomoka kisanii.
Mganga huyo alifunguka kuwa sababu ya kufanya hivyo ni baada ya kuchukuliwa na watu waliompeleka kwa waganga wa Kigoma ambako anajidanganya kuwa ndiyo wanampaisha kumbe walimchukua akiwa ameshampandisha kwa kumpa dawa kali za mvuto.

ALIMPA DAWA GANI?
Alizitaja dawa alizompatia Diamond kuwa ni mitishamba aina ya Dubi, Ntajamasala (hii humfanya watu wamuogope na kumheshimu), Italigula, Nkangacharo na Kalila Lila (ambayo huichoma na kuoga kwa ajili ya kuwavutia watu).

ANGUKO LA DIAMOND
Alidai kuwa Diamond amejisahau na hajui kama anguko lake linakuja kufuatia ahadi aliyoiweka wakati anaanza kuimba baada ya kumpatia dawa hivyo atapotea kwenye muziki.
Akielezea historia ya kukutana kwao, Ustadhi Yahya alisema yeye na staa huyo walikutana miaka ya 2000 nyumbani kwa Papaa Misifa ambaye alikuwa meneja wa Diamond.
Alidai kuwa kubadilika kwa Diamond kulikuja baada ya kutwaa tuzo tatu za Kili mwaka 2010 ndipo akawa anahusudu wanawake tofauti na masharti ya dawa japokuwa alimkanya lakini hakumsikia.

DIAMOND ANASEMAJE?
Kama ilivyo desturi ya gazeti hili, lilimgeukia Diamond ili kupata mzani wa habari hiyo ambapo alipopatikana kwa njia ya simu alisomewa maelezo yake yote.

AMKANA
Katika maelezo yake, Diamond alikataa kata kata kuwa hamfahamu mtu huyo kisha akakata simu.
“Sina msikiti nitakuwaje na Ustadhi? Huyo mganga nasema simfahamu,” alisema kisha akakata simu.

 

source : GLOBAL PUBLISHERS WEBSITE

Views: 4364

Comment

You need to be a member of TEAM TZ to add comments!

Join TEAM TZ

Comment by ISSABELA PATRICK on February 25, 2013 at 3:50pm

lkn!ss watanzania  bwana mtu asifanikiwe

 

Comment by sam juma on February 10, 2013 at 5:09pm

hayo yote maneno ya mkosaj2

Comment by Peter frank on February 8, 2013 at 9:12pm

uongo mtupu

Comment by Johnson Godfrey Chowa on February 6, 2013 at 10:03pm

Au na story hii diamond anataka public attention mana kwa ku tunga vitu hawa masuparstar kawaida tu na kama huamini story hii itaishia hewani

Comment by james machim on February 4, 2013 at 9:17pm

me siwezi kuwa na msimamao wa moja kwa moja ingawa mbea husema ukweli sema tu hajaruhusiwa....ila uchunguz ufanyike zaid huenda kuna ukweli ndani yake.

Comment by Msafiri Sanga on February 3, 2013 at 10:59am
Hana jipya huyo witch dr
Comment by ESSAU NGOBEI on February 3, 2013 at 9:30am

mganga amebandika matangazo bado amekosa wateja sasa amebuni mbinu nyingine ili wanaoanza mziki wamtafute.....kweli hii ni bongo dar es salaaaaammmmmm

Comment by vintan gabriel kantinga on February 3, 2013 at 8:59am
mmmh! hapo mulika mwiiiziiiiii!!!!!!!!
Comment by Mzee Shaban on February 2, 2013 at 7:15pm
Jamani t usikubali wala kukataa
Comment by MIRAJI JUMA HENRY on February 2, 2013 at 5:29pm
Huyu mganga anataka kutengeneza NOMINO kupitia jina kubwa eeenhe,,dogo anaongozwa na uchawi waKIZUNGU nac kivle.......huyo which ajipange

G5 CLICK - LATEST NEWS

EXCLUSIVE - PICHA MPYA ZENYE UTATA ZA DIAMOND PLATNUMZ NA ZARI THE BOSS LADY WAKIWA NDANI YA JIJI LA DAR.

Diamond Platnumz na Zari the boss lady kwa mara ya kwanza walikutana kwenye ndege wakati wakitokea South Africa kuja Tanzania na kupiga picha za kawaida za pamoja ambazo walizi-post kwenye mtandao wa instagram. SASA LEO TEAMTZ.COM…


FREE FLAVA

 

© 2015   Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service