TEAM TZ

Mke na mume wapigana visu baada ya kufamaniana gesti

 SIYO filamu wala igizo, bali ni tukio la kweli lililozua hekaheka katika Kitongoji cha Shekilango, Ubungo jijini Dar es Salaam.


Tukio hilo lililovuta umati mkubwa wa watu ambalo lilishuhudiwa na mwandishi wetu lilitokea Juni 6, mwaka huu saa 11:00 za jioni ambapo mke na mume walikimbizana wakitokea katika Nyumba ya Wageni ya A Plus Lodge, chumba namba 3 huku wakiwa watupu, Gazeti la Amani linakudadavulia kisa kizima.

Wakiwa wanakimbizana, mwanamke akiwa mbele alionekana kushikilia tumbo huku utumbo ukining’inia baada ya kudaiwa kuchomwa kisu na mwanaume huyo.

Mwanamke huyo aliyekuwa akipigania kuinusuru roho yake alikuwa akitoa maneno ya kuomba msaada kutoka kwa wasamaria wema akisema: “ Jamani nisaidieni, mume wangu anataka kuniua, anasema nimemsaliti.”

Hata hivyo, mwanamke huyo hakuweza kufika mbali kwani alianguka chini na baada ya sekunde chache akatokea mume wake, naye akiwa mtupu huku kisu kikiwa kinamning’inia tumboni baada ya kudaiwa kuwa alijichoma.


Haikuchukua muda mrefu umati wa watu ukafika eneo hilo na kupigwa na bumbuwazi juu ya tukio zima, huku wengine wakisema watu hao walikuwa wamefumaniana.
Muda mfupi baadaye askari wa jeshi la polisi walifika eneo la tukio na kuwachukua watu hao, wakawapeleka katika Kituo cha Polisi cha Urafiki na kufungua jalada la kesi namba URP/ RB/ 5126/2011 Mauaji.

Baada ya kumaliza taratibu za kipolisi ndipo watu hao walipopelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na baadaye zikapatikana taarifa kuwa, mwanamke huyo alifariki dunia pale pale huku mwanaume akiendelea kuvuta hewa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camillus Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bado wanalifuatilia na pia alithibitisha kifo cha mwanamke aliyemtaja kwa jina la Happy Samweli au Nyaso anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 27-30.

Hata hivyo, Wambura alisema kwa mujibu wa kitambulisho cha kupigia kura kilichokutwa eneo la tukio, mwanaume huyo ametambulika kwa jina la Lucas John Komba (26), mwenyeji wa Songea, Ruvuma lakini alikuwa amejiandikisha Kiabakari, Kata ya Ukilango, Nyamiskye mkoani Mara.
Polisi imegundua kuwa mke na mume hao waliingia katika nyumba hiyo Juni 5, mwaka huu asubuhi na mwanaume alijiandikisha kwenye daftari la mapokezi kwenye nyumba hiyo ya wageni kwa jina la Abdallah, mkazi wa Tabora.

“Polisi walipofika eneo la tukio na kuingia ndani ya nyumba hiyo ya wageni walizikuta nguo za mwanaume na walipozisachi walikuta barua yenye ujumbe ulioandikwa na mwanaume,” alisema Wambura.
Kwa mujibu wa Wambura, barua hiyo ilikuwa ikimlalamikia mwanamke huyo, Nyaso kuwa amemwambukiza ugonjwa wa Ukimwi na amegundua hilo baada ya kwenda kupima.

Barua hiyo ya Komba iliendelea kudai kuwa, hatua hiyo aliyoichukua ni kwa sababu anaona amepotezewa dira ya maisha na mwanamke huyo.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, Komba bado alikuwa haongei na amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi

 

.

Source : Global Publishers

Views: 349

Tags: Mke, baada, gesti, kufamaniana, mume, na, visu, wapigana, ya

Comment

You need to be a member of TEAM TZ to add comments!

Join TEAM TZ

Comment by frank mibuli kilongola on July 27, 2011 at 4:13pm
mmhh hiyo kali jamani tusichuliane sheria mkononi
Comment by DIARY on July 1, 2011 at 10:53am
Jamani tusimruhusu shetani atutawale kiasi hicho
Comment by josephat minja on June 20, 2011 at 8:26pm
da inasikitisha sana
Comment by CASTUS SIMON on June 15, 2011 at 2:07pm
Sio siri vitu vingine vya kijinga kweli! Inakuwaje mpaka infikia msaliti anamuonea wivu mke au mume ? Kama wanapendana kwann wanasalitiana?Walichotakiwa kufanya ni kuwekwaffair kati yao, wote wakosefu walitakiwa wakubali yaishe.....
Comment by Gabriel Kaliki on June 14, 2011 at 10:23pm
c mchezo iko hot mbaya!!
Comment by faudhiaomary on June 14, 2011 at 5:48pm
dahh! inasikitisha but inafundisha uaminifu jaman
Comment by khalifalism on June 14, 2011 at 4:05pm
du huu ni unyama tosha
Comment by Karim Robert on June 13, 2011 at 1:15pm
duh,inasikitisha sana ila ndiyo maisha
Comment by Albert Lema on June 12, 2011 at 11:57am

uyo mwananke ni evil.. she was supposed to be hanged...

 

Comment by Man Q on June 11, 2011 at 9:34pm

Aiseeeeeee............???????????     It is veeeeeeeeeeeeeeeeeery   Noma...!!!!!!

Daaaah.... Jamaa haangali hata alama za nyakati........anyway ni mtazamo wake..... I hope huo ndiyo mwisho wake wa kufikiria...... The guy does nat even get afraid from God.

Kweli NGOMA nooooooooooooooma kakma ndo hivyo.

G5 CLICK - LATEST NEWS

EXCLUSIVE - PICHA MPYA ZENYE UTATA ZA DIAMOND PLATNUMZ NA ZARI THE BOSS LADY WAKIWA NDANI YA JIJI LA DAR.

Diamond Platnumz na Zari the boss lady kwa mara ya kwanza walikutana kwenye ndege wakati wakitokea South Africa kuja Tanzania na kupiga picha za kawaida za pamoja ambazo walizi-post kwenye mtandao wa instagram. SASA LEO TEAMTZ.COM…


FREE FLAVA

 

© 2015   Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service