TEAM TZ

MWANAMKE TAJIRI NA MREMBO KULIKO WOTE UGANDA

JARIDA  maarufu la  Times nchini  Uganda  limemtaja mama wa watoto wawili Zari Hassan kuwa ndiye mwanamke mrembo na tajiri kuliko wote nchini humo kwa wakati huu.

Kwa  mujibu wa  jarida hilo Zari (30) ambaye ni Mwanamuziki,Mfanyabiashara na Mtangazaji wa  runinga  amepata mafanikio makubwa  kwenye  muziki na pia  kipindi chake cha runinga  kinachofananishwa na  kipindi cha ‘Keeping up with the Kardashians’ kinachoendeshwa na mrimbwende wa kimarekani Kim Kardashian.

Huku likiambatanisha picha za magari na  nyumba  anazomiliki mwanadada huyo, jarida hilo limeandika  kuwa  huenda akaingia kwenye orodha ya wanawake matajiri zaidi Afrika baada ya kipindi kifupi kijacho endapo ataendelea na mwenendo wake wa sasa kibiashara.

hata  hivyo jarida hilo pia  limetaja  zari kuwa mmoja wa mstaa wapenda starehe na  amekuwa  akitumia  mkwanja alionao kumnasa  mwanaume wa aina yoyote anahisi kuwa  anahitaji kumliza kwa wakati huo ingwa tuhuma hizo hazikusibitishwa moja kwa moja.

katika  hatua nyingine jarida hilo limesema  kuwa Zari mwenye maskani yake pia  nchini Afrika ya Kusini, wazazi wake si raia wa uganda kuzaliwa ispokuwa ni wahamiji kwani baba  yake ni raia wa Buurundi mwenye asili ya Somalia na mama yake ni raia wa India kutoka  kabila la Mutoroo.

Views: 2471

Tags: KULIKO, MREMBO, MWANAMKE, NA, TAJIRI, UGANDA, WOTE

Comment

You need to be a member of TEAM TZ to add comments!

Join TEAM TZ

Comment by maroclay on September 25, 2012 at 6:26pm

nice

Comment by Aloyce R xavier.(AMIGO) on August 17, 2012 at 9:45pm

AMETISHA BAAAAAAC

Comment by Emmanuel Yessaya on August 17, 2012 at 4:44am
Eeh vipi madada wa kibongo
Comment by humpa noel godfrey on August 16, 2012 at 8:49pm

ebana eeeeeeeeeeeeee duuuuuuu haya bhna.

Comment by SARAH LYIMO on August 16, 2012 at 11:06am

Nampa pongezi sana. Kwani uleusemi  wa wanaume kusema mwanamke hawezi kufanya chochote cha maendeleo ya kijamii wakomeeeeeeeeee.

G5 CLICK - LATEST NEWS

EXCLUSIVE - PICHA MPYA ZENYE UTATA ZA DIAMOND PLATNUMZ NA ZARI THE BOSS LADY WAKIWA NDANI YA JIJI LA DAR.

Diamond Platnumz na Zari the boss lady kwa mara ya kwanza walikutana kwenye ndege wakati wakitokea South Africa kuja Tanzania na kupiga picha za kawaida za pamoja ambazo walizi-post kwenye mtandao wa instagram. SASA LEO TEAMTZ.COM…


FREE FLAVA

 

© 2015   Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service