Hot Below Trending

Rais Robert Mugabe atangaza amejiuzulu

Rais Robert Mugabe atangaza amejiuzulu
Profile photo of sadock

Spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .

Spika wa bunge Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani ya mamlaka kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng’oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.

Nukuu ya rais Mugabe alipokuwa akijiuzuluHaki miliki ya pichaAFP/GETTY

Image captionNukuu ya rais Mugabe alipokuwa akijiuzulu

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya Jumatano.

Raia wa Zimbabwe wafurahia kujiuzulu kwa MugabeHaki miliki ya pichaAFP

Image captionRaia wa Zimbabwe wafurahia kujiuzulu kwa Mugabe

Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.

Je,ni Kiongozi mkombozi ,mfisadi au mwonevu?

Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung’atuka mamlakani wiki hii.

Amekuwa mamlakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake 1980.

Bwana Mugabe ameshinda uchaguzi wa urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake

Ameongoza kipindi cha uchumi ulioanguka ambapo raia wamezidi kuwa masiki zaidi ya walivyokuwa 1980.

Raia wa Zimbabwe katikati ya mji mkuu wa Harare wakifurahia kuzjiuzulu kwa Mugabe

Hatua iliosababisha yeye kuanza kung’atuliwa madarakani ni ile alipomfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa wiki mbili zilizopita.

Hatua hiyo ilionekana na wengi kama ya kutaka mkewe kumrithi.

Iliwaudhi viongozi wa jeshi ambao waliingilia kati na kumweka rais Mugabe katika kizuizi cha nyumbani.

Ni Shangwe mjini Harare kufuatia kujiuzulu kwa Mugabe

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kuwa kujiuzulu kwa Mugabe kunaipatia Zimbabwe fursa ya kuwa na mwanzo mpya kufuatia ukandamizaji uliotawala uongozi wa Mugabe.

Amesema kuwa Uingereza ambaye ni rafiki wa zamani wa Zimbabwe atafanya kila awezalo kusaidia kufanyika kwa uchaguzi ulio huru na haki na kujenga uchumi wa Zimbabwe.

Rais Robert Mugabe ajiuzuluUbalozi wa Marekani mjini Harare umesema kuwa ni hatua ya kihistoria na kuwapongeza raia wa Zimbabwe kwa kutoa sauti zao na kusema kwa njia ya amani kwamba ni wakati wa mabadiliko.

Chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance kilifurahia hatua hiyo kikisema kuwa bwana Mugabe alibadilika kutoka kuwa mkombozi hadi dikteta.

”Ninafuraha sana leo kwa sababu nimekuwa nikiamini kwamba Mugabe atajiuzulu katika maisha yangu na imefanyika”, alisema mwanaharakati wa haki za kibinaadamu Linda Masarira aliyekuwa akizungumza na BBC.

”Na sasa kwenda mbele ni wakati wa upinzani kujiandaa na kuona kwamba tunakuwa na serikali inayowajali raia wake.Na kila mtu lazima ashirikishwe”.

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017