Hot Below Trending

Saudi Arabia kuwaruhusu wanawake kuingia kwenye viwanja vya michezo

Saudi Arabia kuwaruhusu wanawake kuingia kwenye viwanja vya michezo
Profile photo of sadock

Saudi Arabia itawaruhusu wanawake kuhudhuria michezo katika viwanga vya michezo kwa mara ya kwanza kuanzia mwaka ujao.

Familia zitaweza kuingia kwenye viwanja vitatu vya michezo vya – Riyadh, Jeddah na Dammam.

Ni hatua nyingine ya kuwapa wanawaka wa Saudi Arabia uhuru zaidi, ambao kawaida hukumbwa na ubaguzi wa kijinsia na baada ya kuendolewa marufuku ya kuendesha magari.

Mfalme Mohammed bin Salman yuko katika harakati kubwa kuifanya Saudi Arabia kuwa nchi ya kisasa na kuboresha uchumi.

Mabadiliko hayo yanaambatana na mipango mikubwa ya mabadiliko yaliyotangazwa na mfalme huyo wa umri wa miaka 32 kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kwa taifa hilo linalotegemea mafuta, yanayojulikana kama maoni ya mwaka 2030.

640x392_34736_191107

Mwezi uliopita amri ya kifalme ilisema kuwa wanawake wanaweza kuendesha magari kwa mara ya kwanza kuanzia mwezi Juni mwaka ujao. Warsha zinafanywa na sinema zinatarajiwa kurejeshwa tena.

Siku ya Jumatano Prince Mohammed alisema kurejeshwa kwa uislamu wa wastani ni kiungo muhimu cha kuifanya nchi kuwa ya kisasa.

Alisema kuwa asilimia 70 ya watu nchini Saudi Arabia wana umri wa chini ya miaka 30 na alisema kuwa wanahitaji maisha ambayo yanastahili dini.

Lakini wadadisi wanasema mipango haitakosa pingamiza.

Wanawake nchini Saudi Arabia bado ni lazima wafuate mitindo ya mavazi na wasikuwe na mahusiano na wanaume wasiostahili

BBC Swahili.

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

chrissy-teigen-john-legend-selfie-getty

John Legend na mkewe Chrissy Teigen wanatarajia mtoto wapili

sadockNovember 22, 2017
huhuu

Tiwa savage: Mimi sio mjamzito, hizo ni taarifa za uongo

sadockNovember 22, 2017
clo1

Mkuu wa mkoa, Paul Makonda atembelea ofisi za Clouds Media Group kutoa pole

sadockNovember 22, 2017
pink-beautiful-trauma-tracklist

New Video: P!nk – Beautiful Trauma

sadockNovember 22, 2017