Lifestyle

TAMKO LA MJUMBE WA BODI CHAMA CHA WAIGIZAJI TAIFA KUHUSU WAIGIZAJI KUDHALILISHWA KOROGWE..

TAMKO LA MJUMBE WA BODI CHAMA CHA WAIGIZAJI TAIFA KUHUSU WAIGIZAJI KUDHALILISHWA KOROGWE..
Profile photo of sancho song

Mapema leo tumepokea tamko rasmi kutoka BODI CHAMA CHA WAIGIZAJI TAIFA kuhusiana na uzalilishwaji wa baadhi ya waigizaji huko Korogwe Tanga anaye shutumiwa ni Mr (Jumanne Kiangala)tu

Tuesday Kiangala na hili ndio tamko kutoka kwa mjumbe wa Bodi hiyo

Bi. Lydia Mgaya-Mjumbe wa bodi TDFAA TAIFA Amesikitishwa Sana na Taarifa za Kudhalilishwa na Kunyanyaswa kwa Waigizaji Waliokuwa Kambini Korogwe Kushiriki Moja ya Tamthilia zilizokwenda Kurekodiwa huko.

Ninalaani vikali Vitendo Vinayofanywa na baadhi ya madirector au Viongozi wa Vikundi vya Sana’a Wanaotumia Makundi hayo au hamu na Haja ya Wasanii kufikia Malengo yako Katika Sanaa Kama nyenzo ya Kuwatumia Kingono , Kuwapunja na Kuwanyima kabisa Maslahi , Kuwafanyisha Kazi Kwenye Mazingira Magumu ambayo hayakubaliki Kisheria na Kibinaadamu au Kuwanyanyasa Kwa namna yoyote ile Ikiwamo kijinsia hasa kwa Watoto wa Kike.

Kwa Tukio linalodaiwa Kutokea wilaya ya lushoto mkoani Tanga la kudhalilishwa kwa waigizaji waliokwenda kufanya kazi ya tamthilia ya ndugu Jumanne kihangalla ( Mr.CHUZI ) kama mjumbe anaewakilisha Wasanii wa kike sintokaa kimya kama nilivyoahidi kipindi cha uchaguz, Kulifuatilia Suala hili Kwa Karibu Mno na Kuwataka Waigizaji Wote Wanaotokea Mikoa mbalimbali Tz. Kuripoti Ofisi za Chama mikoani mwao na Kuwasilisha Malalamiko yao Rasmi Kwa Makatibu wao Chama Ili Mchakato wa Kuzuia Tamthilia hiyo Isiruke Mpaka Malipo na HAKI zao Nyingine ziweze Kupatikana.

Hivyo basi ninatoa Pole Kwa Wale Wote Waliofikwa na Madhira Yoyote katika Kadhia hiyo na Kuwaomba Waigizaji Wote Kuwa Makini wakati wa Kuingia Makubaliano Yoyote na Kuacha Kujiona Dhaifu Kutokana na Kiu na hamu yao ya Kutaka Kufanikiwa , Kwa niaba ya Chama Niko tayari Kuwapa Ushirikiano wakati wa Kuingia Makubaliano na Kuwatafutia Msaada Wa Kisheria Ili Kulinda HAKI zao na Kuwapa Usalama wanapokuwa Mahala pao pa Kazi.

Asante.
By Lydia Mgaya.
Mjumbe wa bodi.
Chama Cha Waigizaji Tanzania.
Nakala:
Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo.

Bodi ya Filamu Tanzania.

Shirikisho la Filamu Tanzania.

Chama cha waigizaji Tanzania.

                                                       Chama cha wanawake wa Tasnia ya Filamu.🙏

Comments

comments

Lifestyle

More in Lifestyle

170111_WAR_tillerson.jpg.CROP.promo-xlarge2

Marekani yasema haina uadui na Korea Kaskazini

sadockAugust 2, 2017
kibi

Kibiti Geust House na Viwanja vya panda bei

sancho songJuly 31, 2017
zzzzzzzz

(Eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia),Haya ni baadhi ya yale maneno 68 ya Diamond kwa Zari

sancho songJuly 29, 2017
mazi

Mazishi na muziki -Ghana

sancho songJuly 27, 2017