Hot Below Trending

Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu Marekani

Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu Marekani
Profile photo of sadock

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua mkwe wake Jared Kushner, kuwa mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi hiyo.

Kushner mwenye umri wa miaka 35 ambaye amemuoa binti mkubwa wa Trump, Ivanka, alifanya kazi kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi, zilizomuwezesha Trump kushinda.

jared-kushner-donald-trump

Majukumu ya kazi yake yanatarajiwa kuhusika na masuala ya sera za nje na ndani ya nchi, ikiwemo masuala ya biashara na Mashariki ya Kati.

Uteuzi huo hauhitaji kuthibitishwa na bunge la seneti.

Lakini hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanahoji kama uteuzi huo utakiuka sheria ya kupinga upendeleo wa undugu katika ajira.

Jared Kushner hata chukua mshahara kwa uteuzi huo wa Ikulu ya Marekani na itampa nafasi ya kumfanya kuwa huru na maslahi ya shughuli zake za kibiashara.

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

fu

Trump afuta sheria ya Obama kuhusu walioamua kuegemea jinsia tofauti msalani

sadockFebruary 23, 2017
Mimi Mars

Mimi Mars asema haikuwa rahisi kupata shavu la kusaini kwenye label ya dada yake ‘Mdee Music’

sadockFebruary 22, 2017
uefa

Matokeo ya UEFA jumanne hii: Barcelona yashinda kufurukuta mbele ya PSG

sadockFebruary 15, 2017
MALIA

Video: Obama atoa Hotuba yake ya mwisho kama Rais wa Marekani

sadockJanuary 11, 2017