Hot Below Trending

Tuzo za FIFA 2017: Bao la Olivier Giroud ndilo bora zaidi 2017

Tuzo za FIFA 2017: Bao la Olivier Giroud ndilo bora zaidi 2017
Profile photo of sadock

Bao alilolifunga mchezaji wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Olivier Giroud dhidi ya Crystal Palace limeshinda tuzo ya Bao Bora la Fifa mwaka 2017, maarufu kama Tuzo ya Puskas.

Alifunga bao hilo siku ya Mwaka Mpya katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Kwenye bao hilo maarufu kama ‘scorpion kick’, Giroud aliufikia mpira kutoka kwa mshambuliaji Alexis Sanchez kutoka nyuma yake akaupiga kwa mguu wake wa kushoto na kuupitishia juu ya bega kisha ukaugonga mwamba wa goli kabla ya kutulia kimiani.

Bao hilo la Giroud lilipata kura 36.1% kati ya jumla ya kura 792,062 zilizopigwa.

Giroud alikuwa anashindania tuzo hiyo na Deyna Castellanos wa Venezuela na kipa wa Afrika Kusini Oscarine Masuluke.

Mshindi wa Kombe la Dunia na mshindi wa Serie A mara 10 Gianluigi Buffon ndiye mshindi wa tuzo ya mlindalango bora duniani mwaka huu.

Aliwasaidia Juventus kushinda taji la ligi mara ya sita mtawalia msimu uliopita.

Aidha, alicheza dakika 600 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya bila kufungwa.

Buffon, 39, amewashinda kipa Keylor Navas, wa Real Madrid na Manuel Neuer wa Bayern Munich.

“Ni heshima kubwa sana kwangu kupokea tuzo hii katika umri wangu huu,” alisema Buffon.

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017