Hot Below Trending

Uchaguzi Kenya: Kamishna wa tume ya uchaguzi Kenya Roselyn Akombe IEBC ajiuzulu

Uchaguzi Kenya: Kamishna wa tume ya uchaguzi Kenya Roselyn Akombe IEBC ajiuzulu
Profile photo of sadock

Mmoja wa maafisa wakuu wa Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC) Dkt. Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu katika tume hiyo chini ya wiki moja kabla ya uchaguzi mpya wa urais kufanyika nchini humo.

Dkt Akombe ametuma taarifa kutoka mjini New York anakoishi ambapo alikuwa akiufanyia kazi Umoja wa Mataifa kabla ya kujiunga na tume ya IEBC.

Katika taarifa, Dkt Akombe alisema kuwa merejeleo ya uchaguzi utakaofanyika hayaafikii matarajio ya uchaguzi ulio huru na wa haki.

“Uamuzi wangu wa kuondoka IEBC utawasikitisha baadhi yenu, lakini si kwa sababu nilikosa kujaribu. Nilijaribu kadiri ya uwezo wangu ukizingatia hali na mazingira yaliyopo. Wakati mwingine, unalazimika kusalimu amri na kuondoka, hasa wakati maisha ya watu yamo hatarini,” amesema kwenye taarifa hiyo.

“Tume sasa imekuwa kama sehemu ya mzozo wa sasa. Tume imo matatani.”

“Imekuwa vigumu kuendelea na mikutano ya tume ambapo Makamishna kila wakati wanalazimika kupiga kura kufanya maamuzi kwa kufuata msimamo wao badala ya kuangazia uzito wa jambo linalojadiliwa.

uchaguzi3

“Imekuwa vigumu kutokea kwenye televisheni kutetea misimamo ambayo natofautiana nayo kwa sababu ya kuwajibika kwa pamoja.

“Nimefikia uamuzi kwamba siwezi tena kutoa mchango wa maana kwa Tume na kwa taifa langu kama Kamishna.”

Dkt Akombe alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la maafisa waliokwenda Dubai kuchunguza uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura.

Dkt Akombe alizuru Nyanza na maeneo ya Magharibi, ambayo ni ngome ya upinzani, wiki iliopita huku tume hiyo ikijaribu kuwafunza maafisa watakaosimamia uchaguzi huo.

Wakuu wa IEBC

Mwenyekiti: Wafula Chebukati

Naibu Mwenyekiti: Consolata Nkatha Maina

Makamishna:

  • Boya Molu
  • Paul Kibiwott Kurgat
  • Abdi Guliye
  • Margaret Wanjala Mwachanya

Afisa Mkuu Mtendaji/Katibu: Ezra Chiloba

 

BBC Swahili

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017