Entertainment

Video: Rama Dee amaliza tofauti zake na Clouds FM, awaomba msamaha mashabiki

Video: Rama Dee amaliza tofauti zake na Clouds FM, awaomba msamaha mashabiki
Profile photo of sadock

Mkali wa R&B, Rama Dee hatimaye amaliza tofauti zake na kituo cha radio cha Clouds FM.

Kupitia kipindi cha XXL, Rama Dee ameomba radhi kwa yote yaliyotokea kipindi cha nyuma na kueleza kuwa ni muda wa kufanya muziki mzuri.

“Mimi nasema kwa mashabiki wangu wote wa Clouds Fm na kote wanakonisikiliza, sasa hivi ni muda wa sisi kukaa sehemu moja. Kwa hiyo, kwa chochote ambacho kimetokea kwa Rama Dee ambacho kilionekana si sahihi, naweza kusema I m sorry” Rama Dee alifunguka.

“Na kwa Clouds Fm kwa wao wenyewe wanaona kwamba kuna sehemu walinikosea, tayari tumeshazungumza na tumeshamaliza kwa hiyo tupo sehemu nzuri na bila shaka upendo uendelee,” Aliongeza.

Rama Dee ndiye aliyekuwa akifanya chorus katika ngoma za ‘kundi’ la Anti-Virus ambalo lilitoa albamu za kukishambulia kwa maneno kituo hicho cha radio, hata hivyo Rama Dee amesema katika albamu zilizotoka hakuna sehemu aliyotukana.

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

barnaba

New Video: Barnaba – Mapenzi Jeneza (Official Music Video)

sadockSeptember 20, 2017
future-wizkid-world-tour (1)

New Music: Wizkid f/ Future – Everytime

sadockSeptember 20, 2017
18_ba_ANP-53285975

Uliikosa orodha ya washindi wa tuzo za Emmys 2017, Hii hapa yote

sadockSeptember 20, 2017
atengeneze

Diamond akiri mtoto wa Hamisa ni wa kwake, aomba msamaha

sadockSeptember 19, 2017