Hot Below Trending

Waziri Mwigulu Nchemba asema aliyemtishia bastola Nape sio Polisi lakini ameshapatikana

Waziri Mwigulu Nchemba asema aliyemtishia bastola Nape sio Polisi lakini ameshapatikana
Profile photo of sadock

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema mtu aliyemtishia kwa bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye si askari wa Jeshi la Polisi, lakini ameshapatikana na atashughulikiwa kwa mujibu wa utaratibu wa ulinzi na usalama.

Mwigulu alisema hayo baada ya kufungua mkutano wa kazi wa mwaka wa maofisa waandamizi wa polisi, makamanda wa mikoa na wakuu wa vikosi wa Jeshi la Polisi ambao unafanyika mjini hapa. “Ameshapatikana (aliyemtishia Nape) na atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za ulinzi na usalama ambazo zimekuwa zikifanyika ndani, lakini hazitangazwi,”alisema.

H22A1910

Hata hivyo, Mwigulu alikataa kuelezea kwa undani kuhusu mtu huyo kwa kubainisha anatoka taasisi gani wala jina la mtuhumiwa kwa madai kuwa ni kwa sababu ya usalama wake. Mtu huyo alifanya kitendo hicho wakati Nape, ambaye alikuwa Waziri wa Habari, alipokuwa anaelekea Hoteli ya Protea alikopanga kuzungumza na waandishi wa habari baada ya mbunge huyo wa Mtama kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Mtu huyo alikuwa pamoja na wenzake wawili ambao kwa pamoja walikuwa wakimlazimisha arudi kwenye gari lake na kuondoka, lakini Nape alibisha na ndipo mtu huyo aliporudi nyuma, kuchomoa bastola kutoka kiunoni na kisha kumtishia kabla ya kutulizwa na mwenzake.

Watu hao walitoweka eneo hilo muda mfupi baadaye. Siku moja baada ya tukio hilo Mwigulu alimwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu kumtafuta mtu huyo.

 

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

Daimond1

VIDEO: Diamond ajumuika na watoto wa marehemu IvanDon huko South Africa

sancho songJune 13, 2017
Qatar_Airways_Boeing_777-300ER_A7-BAE_in_special_FC_Barcelona_livery

Misri, Saudi Arabia na Bahrain kufunga anga zake kwa ndege za Qatar

sadockJune 6, 2017
CAF

Watanzania watatu wala shavu la kuwa maofisa waandamizi CAF

sadockMay 16, 2017
imrs

Lionel Messi apigwa na nyundo ya FIFA, Kukosa mechi nne

sadockMarch 29, 2017