Mbali ya Wizkid na Drake kushirikiana kwenye ngoma tatu zilizofanikiwa ikiwemo “One Dance” iliyoongoza chart zote kubwa duniani, Hawajawahi kukutana uso kwa uso.
Mijadala mikubwa imeibuka baada ya Wizkid kuachia video ya ngoma yake mpya “Come Closer” huku rapper wa Canada ambaye ameshirikishwa kwenye ngoma hiyo hajatokea, watu wamehoji huku wengine wakidai kuwa Drake ameamua kupuuzia tu, Wizkid ameamua kujibu sababu ya kwanini Drake hajaonekana kwenye video yake ambapo amesema kuwa wakati anashoot video hiyo Drake alikuwa kwenye Tour yake ya muziki,
“Had a family emergency during one dance shoot and Drake was on tour when we did closer. No bad blood… One love still” Wizkid ameandika Twitter.
Facebook
Twitter
Instagram
YouTube
LinkedIn
RSS