Hot Below Trending

Xavi: Neymar alitaka kujiunga na PSG siku ya harusi ya Messi

Xavi: Neymar alitaka kujiunga na PSG siku ya harusi ya Messi
Profile photo of sadock

Nahodha wa zamani wa Barcelona Xavi amefichua kuwa Neymar alifichua habari za kutaka kujiunga na klabu ya PSG siku ya harusi ya Lionel Messi.

Ripoti za Neymar kutaka kuondoka Barcelona msimu uliopita na kuhusishwa kwake na PSG zilianza kubainika lakini zikashika kas,i na kufikia Agosti 3 Neymar alijiunga na PSG hadi 2022 kwa kitita kilichovunja rekodi ya dunia cha £198m.

Lakini kulingana na Xavi, Neymar alifichua mpango huo mwezi mmoja kabla katika harusi ya Lionel Messi wakati mshindi huyo wa mataji 5 ya mchezaji bora Ballon d’Or alipofunga ndoa na mpenziwe wa miaka mingi Antonella Roccuzzo nchini Argentina.

Messi-Suarez-Neymar

Raia huyo wa Brazil aliwaambia rafikize kuhusu azma yake ya kutaka kuondoka.

Akizungumza na BBC , Xavi ambaye aliichezea Barcelona mechi 700 na kushinda mataji 8 ya La Liga pamoja na makombe manne ya vilabu bingwa Ulaya alisema.

Alituambia siku ya harusi ya Messi kwamba anataka mabadiliko, alitaka kubadilisha klabu na tukamuuliza kwa nini?

Jibu lake alisema ,”kwa kweli sina raha Barcelona,ningependa kupata uzoefu tofauti Ulaya na PSG”.

”Ulikuwa uamuzi wake, lazime tuheshimu”.

”Na nadhani PSG ina kikosi kizuri chini Neymar, Mbappe na wana fursa nzuri ya kushinda kombe la vilabu bingwa Ulaya”.

Tangu uhamisho wake katika mji mkuu wa Ufaransa, Neymar amechezeshwa mechi zote na kufikia sasa amefunga mabao tisa na kutoa usaidizi wa mabao saba na anashirikiana vyema na Kylian Mbappe.

Wakati wa mechi ya klabu bingwa dhidi ya Anderlecht, wawili hao walitoa funzo kuhusu vile soka inavyochezwa.

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017