Entertainment

Z Anto: Kauli ya Lazer ni ya kipuuzi, kwanini achukue muziki wa Nigeria?

Z Anto: Kauli ya Lazer ni ya kipuuzi, kwanini achukue muziki wa Nigeria?
Profile photo of sadock

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Z Anto amesema kauli aliyotoa producer wa WCB Laiza juu ya kusampo biti ya ngoma ya Davido ‘Fall’ na kuitumia katika ngoma ya Diamond ‘Eneka’ ni ya kipumbavu.

Kipindi cha nyuma Laiza alipoulizwa kuhusu hilo alieleza ngoma hizo hazijafanana na hata ikitokea hivyo hamna shida kwani Tanzania haina muziki wake bali inachukua kutoka sehemu mbalimbali.

Muimbaji huyo amesema kauli hiyo ilimuuzi sana kwani Laiza kama producer asingetakiwa kusema hivyo kwani ana uwezo wa kutengeneza kitu chochote kipya.

“Ni kitu ambacho nilikipinga, kama producer ni kauli moja ya kupuuzi mno, wewe producer unaweza kuunda kitu chochote halafu unasema Tanzania hatuna muzki wetu tunawaiga watu fulani haikuwa akauli njema kwa level aliyokuwa nayo, so alikuwa ana uwezo wa kufanya kitu chochote kikawa tofauti” amesema Z Anto.

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Binti Kiziwi’ kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Kacheze Unapochezaga.

Comments

comments

Entertainment

More in Entertainment

chrissy-teigen-john-legend-selfie-getty

John Legend na mkewe Chrissy Teigen wanatarajia mtoto wapili

sadockNovember 22, 2017
huhuu

Tiwa savage: Mimi sio mjamzito, hizo ni taarifa za uongo

sadockNovember 22, 2017
clo1

Mkuu wa mkoa, Paul Makonda atembelea ofisi za Clouds Media Group kutoa pole

sadockNovember 22, 2017
pink-beautiful-trauma-tracklist

New Video: P!nk – Beautiful Trauma

sadockNovember 22, 2017