Hot Below Trending

Zidane baada ya kufungwa na Spurs: Tumefungwa na Timu yenye kikosi bora kuliko chetu

Zidane baada ya kufungwa na Spurs: Tumefungwa na Timu yenye kikosi bora kuliko chetu
Profile photo of sadock

Hapo jana usiku michuano ya Klabu bingwa Barani Ulaya iliendelea katika viwanja mbali mbali huku mabingwa watetezi Klabu ya Real Madrid ikiwa ugenini nchini Uingereza imekubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wao timu ya Tottenham Hotspur.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo meneja wa Madrid, Zinedine Yazid Zidane “Zizou” katika mazungumzo yake na waandishi wa habari amesema kuwa hashangazwi na matokeo aliyopata dhidi ya Spurs kwakuwa timu hiyo ilikuwa imekamilika na bora zaidi kuliko wao.

“Haya ni maisha tu ni ukweli lazima Real ibadilike na kurudi katika kiwango chake ilichokuwanacho hapo hawali,”amesema Zidane anaetambulika kwa jina la utani la Zizou.

Zidane  ameongeza “Hapana sihofii na kamwe sitohofia kwa chochote kitakachotokea msimu huu. Usiku waleo tutafanya uchambuzi lakini tumekutana na timu bora ambayo imekuja kucheza vizuri zaidi yetu lazima tuheshimu hilo.”

totrm011117zg

“Katika upande wa nafasi bado nitasema tumecheza na timu bora  kiujumla na wala sihofii kuona tumekosa magoli tunachohitaji ni kuonyesha kuwa tunauzoefu na ni mabingwa hivyo tutalazimika kubadili muelekeo tunaokwenda nao.”

“Ninachoweza kusema tunapaswa kujilinda na hatuwezi kuwa na furaha na matokeo yaliyopatikana kwa wakati huu mashabiki wetu hawawezi kujiskia vizuri hivyo ni kipindi kibaya kwetu.”

Magoli ya hapo jana usiku katika Uwanja wa Wembley yamefungwa na Dele Alli akiyetupia mawili na Christian Eriksen akipiga moja kwa upande wa Spurs wakati Ronaldo akifunga moja na kupelekea matokeo kuwa 3-1 hivyo Tottenham Hotspur imetinga hatua ya 16 bora.

Wakati Madrid italazimika kushinda michezo miwili iliyobaki ili kupata nafasi ya kuendelea katika michuano hiyo ya klabu bingwa Brani Ulaya.

Comments

comments

Hot Below Trending

More in Hot Below Trending

facup-the-cup-3323603b-1

Ratiba ya raundi ya nne ya FA, Timu ya Nottingham Forest iliyoitoa Arsenal kupambana na Hully City

sadockJanuary 9, 2018
chiiiii

Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Dodoma wathibitisha

sadockJanuary 9, 2018
tottenham_kane_mobile_top

Orodha ya wacheza wenye thamani ya juu zaidi duniani

sadockJanuary 9, 2018
25008524_375147772949765_5376644961137590272_n

Vanessa Mdee aachia cover ya album yake mpya ‘Money Mondays’

sadockDecember 20, 2017